Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Meneja Mawasiliano wa Freconic Ideaz, Krantz Mwantepele (kushoto), akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kampuni yao itaendelea kuleta wanamuziki wengine kutoka pande mbalimbali za dunia kama walivyofanya kwa Robarto Amarula.
Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy kutoka Zambia (kulia), akizungumza na wanahabari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mwanamuziki na mtangazaji wa Redio, Roberto Chindaba Banda 'maarufu Roberto Amarula kutoka nchini Zambia, akifanya vitu vyake mbele ya wanahabari.
Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy, akiimba mbele ya wanahabari. Mwanamuziki huyu atamsindikiza Roberto Amarula wakati wa shoo yao.
Mwanamuziki, Clinton Nyirongo kutoka Zambia naye atakuwepo kutoa burudani.
|
Na Dotto Mwaibale
MWANAMUZIKI wa Zambia anayetamba na wimbo maarufu wa Amarula, Robert Banda ‘Roberto Amarula’, kesho anatarajia kufanya shoo kubwa na ya aina yake katika Ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam kabla ya kufanya hivyo mjini Dodoma kesho kutwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Roberto Amarula, ameahidi kutoa burudanio ya aina yake kwa wakazi wa Dar es Salaam na Dodoma, akiwataka mashabiki wa muziki na burudani kujitokeza kwa wingi kwenye shoo zake hizo.
“Nimefurahia sana kuja Dar es Salaam na ninaahidi kutoa shoo ya aina yake kesho (leo) na Dodoma ili kuwaburudisha Watanzania, lakini pia nitatembelea vituo vya watoto yatima ili kuwafariji na kuwapa nguvu wajione nao ni sehemu ya jamii ya Watanzania na Afrika kwa ujumla,” alisema aliyeambatana na wasanii wenzake wa Zambia, David Banda ‘General Ozzy’ na Clinton Ntirongo ‘Mandela’.
Kwa upande wake, Mkugenzi wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba, alisema kuwa shoo ya leo itawahusisha pia wasanii wa Tanzania kama Ben Pol, Roma Mkatoliki, Fred Swag, Msouth na wengine wengi na kwamba onyesho la Dodoma litafanyika kwenye ukumbi wa Ngalawa Pub, ikiwa ni sehemu ya tamasha la Instagram Party.
Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa Frecon Ideaz, Krantz Mwantepele, alisema: “Tunafahamu kiu ya Watanzania katika suala zima la burudani ndio maana tumewaletea msanii huyu ambaye kwa sasa ni maarufu mno Afrika na kwingineko tukiahidi kuwaleta wasanii zaidi wakubwa Afrika na hata Marekani ili kukata kiu ya mashabiki wa muziki hapa nchini.”
Ziara ya Roberto Amarula ambaye ni mshindi wa tuzo za uandishi bora, mwanamuziki, mtayarishaji muziki na mtangazaji wa redio, iliyoratibiwa kwa pamoja na Freconic Ideaz na C&G Solutions, imedhaminiwa na Millard Ayo, Morena Hotel, Shabiby Bus Servis na Clouds FM. (Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)
No comments:
Post a Comment