TANGAZO


Sunday, November 22, 2015

Zaidi ya wanafunzi 1000 wahitimu katika Mahafali ya Nane ya DUCE jijini Dar es Salaam

Mlau wa Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaama (DUCE) Profesa Martha Qorro akizungumza wakati wa Mahafali hayo yaliyofanyika jana chuoni hapo. Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 1156 walitunukiwa Shahada na Stashahada za juu. 
Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anganisye akitoa taarifa fupi kuhusu mafanikio chuo wakati wa Mhafali ya 8 ya Chuo hicho ambayo yameambatana na maadhimisho ya miaka 10 tangia kuanzishwa kwa chuo hicho jana jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Rwekaza Mukandara akizungumza wakati wa Mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika jana chuoni hapo.  
Baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo jana. 
Mkuu wa Kitivo cha Elimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Dkt. Consolatha Louis Chua akisoma majina ya wahitimu wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo hicho yaliyofanyiki chuoni hapo jana. 
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ,Balozi Nicholas Kuhanga akiwatunuku Shahada wahitimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) (hawapo pichani) alipokuwa mgeni wa Chuo katika Mahafali ya nane ya chuo hicho jana jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. Peter Ngumbulu. 
Baadhi ya wahitimu wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakitunukiwa Shahada zao wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo jana jijini Dar es Salaam. Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 1156 walitunukiwa Shahada. 
Baadhi ya wahitimu wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakifurahia mara baada ya kutunukiwa Shahada zao wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo jana jijini Dar es Salaam. Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 1156 walitunukiwa Shahada na Stashahada za juu. 
Baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakisoma ahadi yao kwa chuo hicho mara baada ya kutunukiwa Shahada na Stashahada ya Juu katika Ualimu wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo hicho yaliyofanyika  jana jijini Dar es Salaam. Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 1156 walitunukiwa Shahada na Stashahada za juu. 
Muhitimu wa mwaka wa tatu ambaye ameongoza kwa ufauli kwa kupata GPA ya 4.8 Bi. Ummul Kheir Mustafa akipongezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. Peter Ngumbulu mara baada ya kupokea zawadi yake ikiwemo kukabidhiwa Cheti chake mbele ya hadhara wakati wa Mahafali ya nane ya chuo hicho jana jijini Dar es Salaam. Muhitimu huyo amekuwa mwanafunzi wa kwanza kunufaika na mpango wa chuo hicho wa kutoa fursa ya kuajiriwa chuoni hapo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katka masomo yao ikiwa ni njia ya kukabiliana na uhaba wa wanataaluma chuo hapo. 
Muhitimu wa mwaka wa tatu ambaye ameongoza kwa ufauli kwakupata GPA ya 4.8 Bi. Ummul Kheir Mustafa akionyesha Cheti chake cmbele ya hadhara mara baada ya kuwa muhitimu wa kwanza kukabidhiwa cheti wakati wa Mahafali ya nane ya chuo hicho jana jijini Dar es Salaam. Mbali na kukabidhiwa Cheti chake cha Shahada papo hapo muhitimu huyo amekuwa mwanafunzi wa kwanza kunufaika na mpango wa chuo hicho wa kutoa fursa ya kuajiriwa chuoni hapo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katka masomo yao ikiwa ni njia ya kukabiliana na uhaba wa wanataaluma chuo hapo. 
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Balozi Nicholas Kuhanga (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu Bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakati wa Mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Lwekaza Mukandara na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Bw. Peter Kuhanga. (Picha zote na Frank Shija, Maelezo)

No comments:

Post a Comment