Wasamaria wema wakisaidia kuokoa magodoro yaliyokuwa yamefukiwa na kifusi kilichotokana na kuvunjwa kwa nyumba na mabanda ya biashara yaliyojengwa isivyo halali kwenye maeneo ya wazi na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, maeneo ya Mwenge jijini leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Kijiko cha Manispaa ya Kinondoni kikivunja moja ya jengo, maeneo ya Mpakani, karibu na ghorofa za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Mwenge jijini leo.
Mkazi wa moja ya majengo yaliyovunjwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, maeneo ya Mwenge jijini leo, Atupokile Mwakasendile, akilalamika kwa waandishi wa habari kuhusu hatua hiyo ya kuvunjiwa nyumba yake.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa wamekaa na baadhi ya vifaa walivyoviokoa.
Kijiko kikivunja gareji, maeneo ya Sinza karibu na Hoteli ya Lion.
Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka Mkuya, akielekeza jambo wakati wa uvunjaji wa gereji kwenye eneo la wazi Sinza jijini leo.
Askari Polisi Kikosi maalum wakiwa katika ulinzi wakati wa zoezi la uvunjaji wa majengo kwenye maeneo ya wazi.
Kijiko cha Manispaa ya Kinondoni kikivunja nyumba iliyojengwa maeneo ya wazi, Mtaa wa Bwawani, Mwananyamala kwa Kopa, Dar es Salaam leo.

No comments:
Post a Comment