TANGAZO


Wednesday, November 18, 2015

Harakati za Wabunge walipokuwa wakila kiapo Bungeni Mjini Dodoma leo

Wabunge wa Songea Mjini (CCM), Leonidas Gama (kushoto), Nzega Vijijini (CCM) Dkt. Hamis Kigwangala (katikati) na Sixtus Mapunda wa Mbinga Mjini (CCM) wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa Bunge hilo leo (Jumatano Novemba 18, 2015). (Picha zote na Hussein Makame)
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na Mbunge wa Viti Maaalum (CCM) Munde Tambwe wakizungumza jambo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa Bunge hilo leo (Jumatano Novemba 18, 2015). 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba (kulia) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Busega Raphael Chegeni nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa Bunge hilo leo (Jumatano Novemba 18, 2015). 
Wabunge wa Viti Maalum (CCM) wakiingia katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma tayari kuanza mkutano wa kwanza wa Bunge hilo leo (Jumatano Novemba 18, 2015. 
Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM) Andrew Chenge (kushoto) na Mbunge wa Mwanga (CCM) Prof. Jumanne Maghembe wakiiingia wakiwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma tayari kuanza mkutano wa kwanzawa Bunge leo (Jumatano Novemba 18, 2015). 
Mbung e wa Viti Maalum kutoka  Chama cha Wananchi (CUF) Riziki Saidi Lulida akiapa kiapo cha Uaminifu.  
Baadhi ya wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF) wakimshangilia mbunge mwenzao Riziki Saidi Lulida bada ya kula kiapo cha Uaminifu. 
Mbunge wa Ilala Musa Azan Zungu akiapa. 
Mbunge wa Butiama Mhe. Nimrod Mkono akiapa. 
Baadhi ya wageni wa wabunge walioapishwa wakiingia na kutoka Bungeni. 
Mbunge wa Arumeru Magharibi Joshua Nassari akiapa. 
Baadhi ya wabunge wakipata maelekezo kutoka kwa mhudumu wa Bunge (kulia). 
Wabunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) Amina Mollel (kushoto) na Stella Ikupa Alex (kulia) akiwasalimiana na mmoja wa wabunge baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge. 

Na Ismail Ngayonga na Lilian Lundo,
Maelezo, Dodoma
17.11.2015
WABUNGE wa mkutano wa kwanza wa kikao cha kwanza cha Bunge la 11 wamemchagua  Job Ndugai (Mb) kuwa Spika wa Bunge la 11 la  Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Ndugai anakuwa Spika wa 7 wa Bunge la Tanzania tangu uhuru, ambaye  alipata kura  254  dhidi ya  kura 109 za mshindani  wake wa  karibu Goodluck  Ole Medeye  kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mhe. Ndungai ambaye ni  mbunge kutoka Jimbo la Kongwa, pia alikuwa  Naibu Spika wa Bunge la Kumi la Jamhuri wa Muungano  wa Tanzania lililokuwa  likiongozwa na Anne Makinda.

Akitangaza matokeo hayo leo (Jumanne Novemba 17, 2015) msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu wa Bunge, Thomas Kashilillah alisema jumla ya kura 365 zilipigwa katika uchaguzi  huo, ambapo kura 2 ziliharibika.

Mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo,  Ndugai alisema ataliongoza Bunge hilo kwa haki na usawa na hivyo kutoa nafasi kwa Wabunge kutoka vyama vyote vya siasa kushiriki katika mijadala mbalimbali ndani ya Bunge.

Aidha Ndugai alisema anafahamu umaskini, mahitaji na matarajio ya Watanzania,  kuhusu nafasi ya chombo hicho katika kuisimamia Serikali, ambayo ni mojawapo ya jukumu la Bunge.
“Namuahidi Mhe. Rais kuwa Bunge hili litakuwa na ushirikiano na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kusimamia kwa karibu shughuli zote  za Serikali ili kunua uchumi wa nchi”
Kwa mujibu wa Ndugai alisema amepata uzoefu wa nafasi hiyo kutoka kwa  Maspika watatu tofauti, ambao ni Pius Msekwa, Samwel Sitta na Anne Makinda, pamoja na kuongoza kamati mbalimbali za Bunge,  hivyo kupitia uzoefu alioupata ataweza kufanya kazi hiyo kwa ufansi zaidi.

Akifafanua zaidi Ndugai alisema ataliongoa Bunge la 11 bila ubaguzi na demokrasia itachukua nafasi yake.

Kwa upande mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Goodluck Ole Medeye alisema hatma ya Watanzania ipo mikononi mwa Bunge hilo, hivyo wabunge hawana budi kutoa ushirikiano kwa Spika ili aweze kutimiza wajibu wake.

Wakiongea kwa wakati tofauti, wagombea wengine wa kinyang’anyiro cha nafasi hiyo, walitoa pongezi kwa Spika Ndugai na kumtaka kulifanya Bunge kuwa chombo chenye kuwaunganisha Wabunge wote na kuondoa misuguano na tofauti ya vyama ndani ya Bunge.

Jumla ya Wagombea 8 kutoka vyama vya AFP, CHADEMA, CCK, NRA, CCM, TLP, CHAUMMA, na DP  waliwania nafasi hiyo, huku mgombea kutoka CHAUMMA, Hashim Rungwe akishindwa kutoka kufika katika uchaguzi huo pasipo na kutoa taarifa kwa msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Katibu wa Bunge.


Hata hivyo Wagombea  kutoka katika vyama sita ambavyo ni AFP, CCK,NRA, TLP, CHAUMMA na DP hawakuweza kupata kura yoyote kati ya kura halali 363.

No comments:

Post a Comment