TANGAZO


Saturday, November 21, 2015

Serikali za Mitaa zaongeza mapato kupitia mfumo wa ukusanyaji kwa njia ya kielektroniki

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI Bi. Rebecca Kwandu akifurahia jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dar es Salaam wakati akiwaeleza mafanikio ya mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki katika mamlaka za Serikali za Mitaa (LGRCIS). Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Mifumo ya TEHAMA wa ofisi hiyo Bw. Mtani Yangwe na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa. 
Mkurugenzi Msaidizi Mifumo ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI Bw. Mtani Yangwe akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jana, jijini Dar es Salaam namna mfumo wa wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki unavyorahisisha ulipaji wa kodi mbalimbali kwa kuhusisha mifumo ya kielektroniki ya malipo na mifumo ya kibenki. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa ofisi hiyo Bi. Rebecca Kwandu. 
Ofisa Msimamizi wa Fedha Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI Bw. Elisa Rwamiago akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) jana, Dar es Salaam kuhusu mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato ya mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuondokana na utegemezi wa ruzuku kutoka Serikali Kuu. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa ofisi hiyo Bi. Rebecca Kwandu. 
Mhasibu wa Mfumo wa Mapato Jiji la Arusha Bw. Prosper Mlacha akiwaeleza waandishi wa habari jana, Dar es Salaam kuhusu ongezeko la mapato katika jiji la Arusha kutokana na matumizi ya mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki (LGRCIS) ambapo kwa mwaka 2014/2015 zimekusanywa bilioni 10.7. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI uliofanyika jana, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Fatma Salum-Maelezo)

No comments:

Post a Comment