Mwenyekiti wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI) Dar es salaam Bw. Harith
Shomvi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo akihutubia wananchi
na kuwasisitiza wapate huduma za uzazi wa mpango na upimaji ambazo zilikuwa
zikitolewa bure katika tamasha hilo. Tamasha hilo lilikuwa na kauli mbiu
isemayo "JE kutoa elimu juu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa
vijana ni jukumu la nani?
Vijana wa YAM (Youth Action Movement) ambao ni
waandaaji wa tamasha hili linalofanyika kila mwezi wakionesha igizo lao
lililobeba ujumbe unaosema ni jukumu la wazazi kuwaelimisha vijana juu ya afya
ya uzazi na ujinsia ili kuwakinga na maambukizi ya VVU mimba katika umri mdogo
na ngono katika umri mdogo.
Vijana wa YAM (Youth Action Movement) ambao ni waandaaji wa tamasha hili linalofanyika kila mwezi wakionesha igizo lao lililobeba ujumbe unaosema ni jukumu la wazazi kuwaelimisha vijana juu ya afya ya uzazi na ujinsia ili kuwakinga na maambukizi ya VVU mimba katika umri mdogo na ngono katika umri mdogo.
Baadhi ya wananchi wakijiandikisha ili waweze
kupata huduma ya upimaji VVU na uzazi wa mpango zilizokuwa zikitolewa bure na
UMATI katika tamasha hilo la jamvi la vijana.
Mtoa huduma wa UMATI Bibi. Neema Orgeness
akimpima mteja VVU.
Mtoa huduma wa UMATI Monika Nkwera akimpatia
mama huduma ya uzazi wa mpango wakati wa Tamasha la Vijana lililofanyika
jijini Dar es Salaam mapema wikiendi hii. Tamasha hilo lilikuwa na kauli mbiu
isemayo "JE kutoa elimu juu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa
vijana ni jukumu la nani?
Kikundi
cha nyota kutoka Temeke wakionesha igizo linaloelezea umuhimu wa wazazi kuwapa
elimu ya afya ya uzazi na ujinsia watoto wao ili kuwaepusha na ngono katika
umri mdogo,mimba katika umri mdogo,VVU/UKIMWI,na pia athari zingine zitokanazo
na ukosefu wa elimu na habari sahihi kuhusu afya ya uzazi na ujinsia. (Picha zote na Frank Shija, WHVUM)








No comments:
Post a Comment