TANGAZO


Thursday, November 26, 2015

Covenant Bank yatoa sh. milioni 10 mapambano dhidi ya saratani ya matiti

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  ya Covenant Bank,  Balozi Salome Sijaona (katikati) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi, Kwa wawakilishi wa  Taasisi ya Tanzania Breast Cancer, kutoka kushoto Meneja Mradi wa taasisi hiyo Kisa Mwakatobe na mweka Hazina wa taasisi hiyo ambae pia ni Mhanga wa Saratani ya Matiti Gloria Kida, fedha hizo ilizotolewa na benki hiyo zitatumika katika kununua matiti ya bandia pamoja na vifaa tiba vingine kwa wanawake wenye saratani. Pamoja nao kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank,  Sabetha Mwambenja na Meneja Fedha, Patrick Kyamba. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  ya Covenant Bank,  Balozi Salome Sijaona (katikati) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi, Kwa wawakilishi wa  Taasisi ya Tanzania Breast Cancer, kutoka kushoto Meneja Mradi wa taasisi hiyo Kisa Mwakatobe na mweka Hazina wa taasisi hiyo ambae pia ni Mhanga wa Saratani ya Matiti Gloria Kida, fedha hizo ilizotolewa na benki hiyo zitatumika katika kununua matiti ya bandia pamoja na vifaa tiba vingine kwa wanawake wenye saratani. Pamoja nao kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank,  Sabetha Mwambenja na Meneja Fedha, Patrick Kyamba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, wa kwanza kulia, akizungumza na waandishi wa  habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi  fedha kwa ajili ya kupambana na saratani ya matiti. Benki hiyo imechangia Milioni kumi kwa ajili ya kununu matiti  bandia kwa wanawake wenye saratani  pamoja na kugharamia matibabu yao.  Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salome Sijaona, Meneja Miradi wa Tanzania Breast Cancer foundation, Kisa Mwakatobe na Mweka Hazina wa Taasisi hiyo. Gloria Kida.
Baadhi ya waandishi wa habari na wageni waalikwa waliojitokeza katika hafla hiyo.


Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam 26, Novemba 2015, 
KATIKA kuhakikisha inaendeleza mapambano dhidi ya saratani ya matiti ambayo imekuwa ikipoteza maelfu ya maisha ya wanawake nchini Benki ya Covenant imechangia kiasi cha Shilingi milioni kumi kwa taasisi ya Tanzania Breast Cancer, ambayo inajihusisha na mapambano ya ugonjwa huo ikiwa ni sehemu ya kuongeza nguvu katika mapambano ya ugonjwa wa saratani.

Akizungumza kabla ya kukabidhi hundi ya fedha hizo,  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Balozi, Salome Sijaona, amesema benki yake inaguswa na matatizo mbalimbali yanayowakabili Watanzania hususani wanawake ambao wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo saratani ya matiti na shingo ya uzazi ambayo imekuwa ikiwatesa mamia ya wanawake nchini.

“Tunaguswa na matatizo yanayowakabili wanawake wa Tanzania, haswa ugonjwa wa saratani ya Matiti na shingo ya uzazi, ugonjwa huu umekuwa na mateso makubwa kwa wanawake wa Tanzania ambao wengine ni wateja wetu, Tumeguswa na tumeona ni vyema tutoe kiasi hiki kidogo  ambacho kinaweza kusaidia kupunguza mateso haya, alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa.

“Kiasi hiki kinaweza kuwa kidogo ukilinganisha na hali halisi ya tatizo la Saratani ya Matiti na Shingo ya uzazi nchini  ila tutaendelea kuangalia namna gani tunaweza kuendelea kutoa msaada kwa wanawake hawa, kulingana na uwezo tulionao, hivyo nichukue fursa hii kuwaomba wadau wengine kujitokeza na kuchangia dhidi ya mapambano ya ugonjwa huu” Alisema Balozi Sijaona.

Awali akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya benki hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja amesema kuwa, wataendelea kuchangia mapambano dhidi ya ugonjwa  saratani ya matiti na shingo ya uzazi, huku akisikitishwa na wanawake wenye matatizo ya ugonjwa huo kukosa bima ya Matibabu ambayo ingewawezesha kukabiliana na gharama kubwa za matibabu.

Aidha Meneja Miradi wa Taasisi ya Tanzania Breast Cancer, Kisa Mwakatobe, pamoja na kuishukuru Covenant Bank kwa kutoa fedha hizo amesema kuwa msaada huo utasaidia kuchangia matibabu kwa baadhi ya wanawake ambao wanakosa fedha kwa ajili ya matibabu, kutembeea wagonjwa na kuwapa ushauri katika mahospitali mbalimbali na majumbani kwao pamoja na kununua matiti ya bandia (artificial breast) kwa wanawake wenye uhitaji.

“Tunashukuru kwa msaada huu, mkubwa ambao tumeupata, fedha hizi zitasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake wenye ugonjwa wa saratani” alisema Mwakatobe na kuongeza.

“Tatizo la saratani ya matiti na shingo ya uzazi ni kubwa sana nchini na zinahitajika nguvu za ziada katika kukabiliana na tatizo hilo kwani sasa linawatokea hata mabinti walioko katika umri kuanzia miaka kumi na tano na kuomba jamii ijitolee kukabiliana na ugonjwa huo kwa kujitokeza kushiriki katika matembezi ya hiri ya kilometa tano katika kuchangia fedha kwa ajili ya mapambano ya ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment