TANGAZO


Monday, October 5, 2015

Shinikizo Somalia iwaachilie wanahabari



Image captionNicholas Kay, amesema kwamba kuzuiliwa kwa mtangazaji Awil Dahir Salad na msimamizi Abdullahi Hersi, ni tishio kwa uhuru wa vyombo vya habari.

Serikali ya Somalia inakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa jamii ya kimataifa kuwaachilia huru waandishi wawili wa habari waliokamatwa siku ya Ijumaa.
Wawili hao walitiwa mbaroni baada ya kituo chao cha habari cha Universal TV kupeperusha hewani mjadala wenye utata.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay, amesema kwamba kuzuiliwa kwa mtangazaji Awil Dahir Salad na msimamizi Abdullahi Hersi, ni tishio kwa uhuru wa vyombo vya habari.


Image copyrightAP
Image captionKunashauku huenda mjadala mkali kuhusu hatua ya kutaka kumn'goa rais Hassan Sheikh Mohamud madarakani ndiyo iliyowachongea.

Kundi moja la wanaharakati la kuwatetea wanahabari liitwalo Reporters Without Borders, limetaja hatua hiyo kuwa yenye nia ya kuvikandamiza vyombo vya habari.
Washiriki katika mjadala huo walikosoa serikali kwa kukubalia majeshi ya Kenya na Ethiopia kuingia nchini Somalia ili kukabiliana na wanamgambo wa makundi ya Kiislamu.
Hata hivyo kuna wanaodai huenda mjadala mkali kuhusu hatua ya kutaka kumng'oa rais Hassan Sheikh Mohamud madarakani ndiyo iliyowachongea.

No comments:

Post a Comment