TANGAZO


Wednesday, September 16, 2015

Rais Kikwete azindua Jengo refu kabisa la PSPF Tower lenye ghorofa 30 jijini Dar es Salaam leo


Kikundi cha ngoma za asili cha Mjomba Band, kikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF, jijini Dar es Salaam leo. Uzinduzi wa jengo hilo, umefanywa na Rais Jakaya Kikwete. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Gwiji wa muziki wa dansi, Mzee Kassim Mapili (katikati), akipiga gita la Solo huku akiimba, alipoiongoza Mjomba Band, kutumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF, jijini Dar es Salaam leo. Uzinduzi wa jengo hilo, umefanywa na Rais Jakaya Kikwete.   
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati alipowasili kulizindua jengo la mfuko huo la 
Rais Jakaya Kikwete, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya hafla hiyo.
Viongozi na wageni mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki.
Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa PSPF, Adam Mayingu (kulia), wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo hilo, jijini leo. 
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza wakati alipozindua jengo hilo, la PSPF jijini leo.  
Rais Jakaya Kikwete, akisaini fomu maalum za unachama wa uchangiaji wa hiyari wa Mfuko wa PSPF, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa jengo hilo, jijini leo.  
Rais Jakaya Kikwete, akiweka alama ya dole gumba kwenye fomu hizo, maalum za unachama wa uchangiaji wa hiyari wa Mfuko wa PSPF, wakati wa hafla hiyo leo.  
Rais Jakaya Kikwete, akikabidhiwa mfano wa kadi ya uanachama wa uchangiaji wa hiyari na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa PSPF, George Yambesi. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima. 
Rais Jakaya Kikwete, akikabidhiwa mfano wa kadi ya uanachama wa uchangiaji wa hiyari ya mkewe, Mama Salma na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa PSPF, George Yambesi. Kulia anayefurahia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima.  
Rais Jakaya Kikwete, akikabidhiwa picha ya jengo hilo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa PSPF, George Yambesi. Kulia anayepiga makofi ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima.
Rais Jakaya Kikwete, akikata utepe wakati akizindua jengo la PSPF Tower, lililopo makutano ya Barabara za Mission na Sokoine, Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa PSPF, George Yambesi na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa PSPF, Adam Mayingu.
Rais Jakaya Kikwete, akifunua pazia wakati akizindua jengo la PSPF Tower, lililopo makutano ya Barabara za Mission na Sokoine, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akipiga makofi mara baada ya kufunua pazia wakati akizindua jengo la PSPF Tower, lililopo makutano ya Barabara za Mission na Sokoine, Dar es Salaam leo. Kushoto anayepiga makofi ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa PSPF, George Yambesi.  
Rais Jakaya Kikwete, akipiga picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Mfuko wa PSPF, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa jengo hilo, jijini leo.  
Rais Jakaya Kikwete, akikagua sehemu mbalimbali za ndani ya jengo hilo, mara baada ya kulizindua jengo hilo lililo refu kabisa Afrika Mashariki na Kati, lenye ghorofa 30.
Kikundi cha ngoma na sarakasi cha Mjomba Band, kikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF, jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment