TANGAZO


Tuesday, September 8, 2015

Msemaji wa upinzani auawa Burundi

Image copyrightAFP
Image captionPatrice Gahungu wa chama cha Union for Peace and Development aliuawa alipokuwa akiendesha gari kwenda nyumbani kwake siku ya jumatatu usiku.
Msemaji wa chama cha upinzani nchini Burundi ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa Bujumbura.
Patrice Gahungu wa chama cha Union for Peace and Development aliuawa alipokuwa akiendesha gari kwenda nyumbani kwake siku ya jumatatu usiku.
Kiongozi wa chama hicho Zedi Feruzi naye aliuawa kwa kupigwa risasi mwezi Mei wakati wa maandamano ya kumpinga rais Pierre Nkurunziza.
Watu wengine wawili waliuliwa hapo jana mjini Bujumbura lakini polisi bado wanaendelea na uchunguzi.
Image captionMaandamano hayo yaliitishwa na upinzani kupinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Maandamano hayo yaliitishwa na upinzani kupinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Watu kadha wameuawa na maelfu ya wangine wameikimbia nchi hiyo tangu kuzuka kwa mzozo mwezi Aprili.

No comments:

Post a Comment