TANGAZO


Tuesday, September 8, 2015

Bomu laua polisi 10 Uturuki

Image copyrightAFP
Image captionGari lisilopenya risasi liliharibiwa kabisa
Takriban polisi 10 wa Uturuki wameripotiwa kuuawa katika shambulio la bomu lililotegwa ndani ya basi dogo mashariki mwa nchi hiyo .
Shambulio hilo limetokea siku mbili baada ya shambulio jingine dhidi ya magari ya kijeshi ya Uturuki kusini magharibi mwa nchi hiyo lililowauwa askari 16.
Image captionNdege za kijeshi za Uturuki zimelipua maeneo yanayokaliwa na PKK Iraq
Maafisa wamewalaumu wapiganaji wa kundi la kikurdi la PKK kwa mashambulio hayo .
Wakati huo huo ndege za kijeshi za Uturuki zimefanya mashambiulizi zaid ya uvamizi dhidi ya ngome za PKK nchini Iraq.
Image captionShambulizi la awali liliwaua wanajeshi 16
Vyombo vya habari vya Uturuki na maafisa wa usalama wanasema ndege zaidi ya arobaini zimefanya mashambulizi na kuharibu handaki na maghala ya chakula ya PKK.

No comments:

Post a Comment