TANGAZO


Monday, September 7, 2015

Msajili wa Vyama vya Siasa asema hakuna Chama cha siasa kinachoitwa TPP kinachoshiriki Uchaguzi Mkuu

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya waandishi wa habari na wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari, wakiwa kwenye mkutano na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, jijini Dar es Salaam leo. 
Msaidizi wa Msajili wa Vyama Vya Siasa, Sisty Nyahoza akizungumza na waandishi wa habari leo, kwenye ukumbi wa mkutano wa ofisi hiyo, jijini Dar es Salaam kuhusu vyama vyenye usajili wa kudumu ambavyo vinastahili kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. 
Msaidizi wa Msajili wa Vyama Vya Siasa, Sisty Nyahoza akizungumza na waandishi wa habari leo, kwenye ukumbi wa mkutano wa ofisi hiyo, jijini Dar es Salaam kuhusu vyama vyenye usajili wa kudumu.
Msaidizi wa Msajili wa Vyama Vya Siasa, Sisty Nyahoza akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kuhusu vyama vyenye usajili wa kudumu ambavyo vinastahili kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Msaidizi wa Msajili wa Vyama Vya Siasa, Sisty Nyahoza akizungumza na waandishi wa habari leo jijini leo, kuhusu vyama vyenye usajili wa kudumu ambavyo vinastahili kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. (Picha zote na Magreth Kinabo-MAELEZO)

Na Magreth Kinabo –MAELEZO
OFISI ya Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini imesema kwamba hakuna chama cha siasa chenye usajili wa kudumu au wa muda kinachoitwa Tanzania Peoples Party(TPP) kinachoshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya Vyama Vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992.

Aidha Ofisi hiyo imesema kwamba hivi sasa kuna vyama  22 ndivyo vinavyoshiriki katika uchaguzi huo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Msaidizi wa Msajili wa Vyama Vya Siasa, Sisty Nyahoza,wakati akizungumza na waandishi wa habari leo  kwenye ukumbi wa mkutano wa ofisi hiyo jijini Dar e s Salaam kuhusu vyama vyenye usajili wa kudumu ambavyo vinastahili kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Nyahoza alifafanua hayo kutokana na kuwepo kwa taarifa katika  gazeti moja la habari hapa nchini, ambalo Septemba 4 ,mwaka huu liliripoti  kwa kutumia picha na  maneno kuhusu chama hicho katika toleo namba 0455 ukurasa wa tatu.

“Chama hiki kilikiuka katika kwa mujibu wa sheria kwa sababu kilikiuka masharti ya  usajili wa vyama vya siasa,” alisema Nyahoza.

Kwa mujibu wa Nyahoza alisema hicho kilifutwa kutokana na sababu ya kukosa kiongozi kwa kuwa sheria hiyo katika kifungu cha 9 kinasema chama cha siasa kiwe na uongozi wa kitaifa.

Hivyo mwaka 2002 kilishindwa kuchagua viongozi wa chama kwa sababu ya kutokuelewana. 

Nyahoza aliongeza kwamba chama hicho, awali kilisajiliwa mwaka 1993 baada Ya kukidhi masharti, lakini kilifutwa kwenye orodha ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu na Msajili wa Vyama Vya Siasa Machi 20, mwaka 2002. Hivyo sasa hivi hakipo kwa mujibu wa sheria.

“ Hivyo hivi sasa hakipo kwa mujibu wa Sheria. Kifungu cha 7(3) cha Sheria   ya Vyama Vya Siasa sura ya 358  kinakataza taasisi yoyote kufanya kazi kama chama cha siasa bila kusajiliwa na Msajili wa Vyama Vya  Siasa,” alisema.

Aidha  kifungu cha 8(b) cha sheria hiyo kama ilivyorekebishwa mwaka 2009 kinakataza mtu yoyote kufanya shughuli za kisisa kwa jina la chama ambacho yeye si mwanachama au kiongozi.

Alisema wanaokika  vifungu vya sheria hiyo waelewe kuwa wanafanya kosa la jinai, hivyo wanaaswa kuacha  mara moja. Pia amewaasa wananchi, wanachama na viongozi wote wa vyama vya siasa  kuheshimu na kutii sheria za nchi ili uchaguzi uweze kufanyika vizuri kwa amani na utulivu.

Vyama vinavyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu  wa mwaka  huu ni CCM, CUF,CHADEMA, UMD,NCCR- Mageuzi, NLD,UPDP,NRA, TADEA,TLP,UDP,DEMOKRASIA MAKINI,CHAUSTA,DP,APPT-Maendeleo,Jahazi Asilia,SAU,AFP,CCK,ADC,CHAUMMA, na ACT.

No comments:

Post a Comment