TANGAZO


Thursday, September 10, 2015

Mamlaka ya Elimu Tanzania yatoa ufadhili wa milioni 300 kwa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mwalimu Julius K. Nyerere

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bw. Joel Laurent akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu mikakati ya mamlaka hiyo, katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini kupitia Mfuko wa Elimu. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mwalimu Julius K. Nyerere, Prof. Dominic  Kambarage. 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mwalimu Julius K Nyerere, Prof. Dominic Kambarage (wa pili kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bw. Joel Laurent (wa pili kulia), wakitiliana saini makubaliano ya ufadhili wa shilingi millioni 300, utakaotolewa na TEA kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi na kutengeneza mtaala katika Kampasi ya Butiama ya Chuo Kikuu cha Sayansi naTeknolojia cha Mwalimu Julius K Nyerere. Hafla hiyo fupi mefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Msafiri Jackson na kulia ni Mkurugenzi Uratibu na Ufadhili Miradi wa TEA, Bibi Anna Magalla. 
MakamuMkuuwa Chuo Kikuu cha SayansinaTeknolojia cha Mwalimu Julius K Nyerere Prof. Dominic Kambarage akitoa shukrani kwa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa ufadhili wa Sh. millioni 300 utakaotolewa na mamlaka hiyo, kusaidia Ujenzi wa jengo la Ofisi za Utawala na wakufunzi pamoja na ununuzi wa samani za Ofisi hizo na utengenezaji wa mtaala kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bw.Joel Laurent. 
MakamuMkuuwa Chuo Kikuu cha SayansinaTeknolojia cha Mwalimu Julius K Nyerere Prof. Dominic Kambarage (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent (kulia), wakikabidhiana hati za makubaliano ya ufadhili wa sh. millioni 300, utakaotolewa na TEA kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi na kutengeneza mtaala katika Kampasi ya Butiama ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mwalimu Julius K. Nyerere kwenye hafla fupi iliyofanyika leo, jijini Dar es Salaam. Katikatini Prof. Lesakit Mellay Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma na Utafiti. 
AliyekuwaNaibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Philip Mulugo akipokea zawadi ya kumbukumbu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bw. Joel Laurent wakati alipotembelea ofisi za mamlaka hiyo, leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa TEA, Bibi Sylvia Lupembe.
AliyekuwaNaibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Philip Mulugo (wanne kushoto), akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), wakati alipotembelea ofisi za mamlaka hiyo, leo jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bw. Joel Laurent. 
Wakuu wa Idara mbalimbali za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakifurahia jambo na aliyekuwa Naibu Waziri waElimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Philip Mulugo (katikati), nje ya Ofisi za mamlaka hiyo, leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bw. Joel Laurent. (Picha zote na Fatma Salum (MAELEZO)

No comments:

Post a Comment