Kundi la Karafuu Band likitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), uliohutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na wanaCCM, wananchi na wapenda amani katika Wilaya ya Kaskazini A, Jimbo la Tumbatu katika Uwanja wa Sunrize, Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja leo jioni.
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
VIONGOZI wa CCM Zanzibar wameeleza kuwa hoja inayotolewa na chama cha CUF ya
kutaka kuleta Mamlaka Kamili ni dhamira ya kumrejesha Sultan kuja kuiongoza
Zanzibar kwa njia ya mlango wa nyuma.
Viongozi hao waliyasema hayo leo katika
Mkutano wa Kampeni ya uchaguzi wa CCM
uliofanyika katika Uwanja wa Sun Rise, Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja
uliohudhuria na maelfu ya wanaCCM na wananchi ambapo mgeni rasmi alikuwa
mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein.
Alisema kuwa CUF hawana hoja na
kushangazwa na kauli inayotoa kuwa Zanzibar haina Mamlaka kamili wakati tayari
Zanzibar inayo mamlaka Kamili ila nia ya chama hicho ni kurudisha uongozi wa
Kifalme.
Alisema kuwa viongozi wa CUF wameishiwa
hoja na hawana la kuwaambia wafuasi wao na hivi sasa wamekuwa wakitumia jina
lake kwa kunokesha mikutano yao. "labda kwa kwa sababu mimi mweusi na siwezi
kujifanya mweupe kama Jusa",alisema Balozi Seif.
"Kama mimi mweusi ndio alivyoniumba
Mungu sasa na wale waliokuwa na vilema visivyoonekana inakuwaje",alisema
Balozi na kueleza mwaka huu CUF wanaanguka
huku akisisitiza kuwa Serikali inatolewa kwa nguvu za kura.
Aidha, Balozi Seif Ali Idd, alisema kuwa
CUF hawana ajenda na liliopo hivi sasa ni kubwabwaja na kuwaeleza wanaCCM
kilichobaki ni kwenda kupiga kura tarehe 25 mwezi huu, na CCM kupata ushindi na
kueleza kuwa CUF haina ubavu wa kuishinda CCM.
Balozi Seif alisema kuwa tayari chama cha
CUF wanajua kuwa mara hii wanashindwa na
ndio maana wamekuwa wakipita kununua vitambulisho vya kupigia kura kwa
wanaCCM.
Alieleza kuwa mikakati wanayopaka ya
kufanya vurugu Oktoba 24, 25 na 26, tayari imeshajulikanwa na kutumia fursa
hiyo kuwata wazee wa CUF wa Mkoa wa Kaskazini kutowaachia watoto wao kufanya
vurugu na kusema kuwa vyombo vya dola havichezewi na kuwataka wasije wakailaumu
Serikali na kutowaachia watoto wao kuingia mtegoni, wasije kufanya vuru, wala
maandamano.
Alisema kuwa mambo mengi ya vurugu wanayokusudia
kufanya CUF wanayajua na wana ushahidi nayo na huku akieleza kuwa ipo siku
watayatoa. "Chokochoko kachokoe pweza...CCM haichokolewi iko imara na
ukifanya mchezo itakushughulikia",alisema Balozi Seif.
Alisema kuwa Oktoba 25 mwaka huu ni siku ya ushindi wa CCM hivyo kila
mmoja aende mapema kupiga kura na kuwahakikishia wananchi kuwa siku ya uchaguzi
ulinzi wa kutosha utakuwepo kwa ajili yao na watalindwa wakati wote.
Nae Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri
Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai Nahodha alisema kuwa Mamlaka kamili ya Zanzinar yalipatikanwa
tokea mwaka 1964 chini ya Marehemu Mzee Abeid Karume na hakuna mtu yeyote wala
kikundi chochote cha watu ambacho kina uwezo wa kufanya hivyo hivi leo.
Alisema kuwa wanachokusudia kukifanya
chama hicho kwa kutaka Zanzibar iwe mwanachama wa Umoja wa Mataifa, iwe na safaru
yake, Wizara yake ya mambo ya nje yake ni jambo la kushangazwa kwani taifa
lolote duniani haliwezi kuwa na viti viwili katika umoja wa Mataifa wala
haiwezekani kuwa na sarafu mbili wala Wizara mbili za Mambo ya nje ndani ya
taifa moja.
Shamsi aliendelea kushangazwa na CUF kutaka
kuanzisha Mamlaka kamili na kueleza kuwa chama hicho na kile cha CHADEMA msimamo wao unafanana
lakini dhamira zinatofautiana kwani lengo lao ni kuvunja Muungano kwa kutumia
lugha ya ulaghai.
Alisema kuwa dhamira ya CHADEMA ni
kuwarubuni CUF ili kuwaunga mkono na kuwa na mgombea mmoja wa Jamhuri ya
Muungano na la kusikitisha zaidi ni kuwa CHADEMA kimefanikiwa, kuvidhoofisha vyama
vya CUF na NCCR-MAGEUZI. Pia alieleza kuwa CCM itaendelea kuunga mkono sera ya
Serikali mbili.
Alieleza kuwa CCM inaamini kuwa Sera ya
Serikali mbili ndio yenye uwezo wa kuongoza serikali, na kusisitiza kuwa Sera
ya Serikali tatu haina uwezo wa kuulinda Muungano wala kuyalinda Mapinduzi ya
Januari 12, 1964.
Kwa upande wa Muungano alisema kuwa
Wazanzibari wamekuwa wakinufaika na Muungano na kueleza kuwa Tanzania Bara wapo
Wazanzibari wanaopata huduma kadhaa za maisha ya mwanaadamu ikiwemo ardhi, maji
safi na salama na huduma nyenginezo bila
ya bughudha.
Shamsi alishangazwa na wale wote
wanaosema kuwa Muungano hauna maana na kueleza kuwa ipo haja ya kutafuta mada
nyengine na sio hiyo.
Akieleza juu ya vitendo vinavyofanywa na
viongozi wa CUF, alisema kuwa wapo wanachama na viongozi wanapita kwenye
Majimbo kununua vitambulisho vya kupigia kura na kueleza kuwa Sheria ya
uchaguzi inasema kuwa mwananchi yeyote wa Zanzibar aliyesajiliwa kwenye Daftari,
haijalishi kuwa shahada yake, imepotea ama imenunuliwa au imeibiwa, ana haki ya
kupiga kura.
Hivyo aliiomba Tume ya Uchaguzi
kuhakikisha kila Mzanzibari mwenye Shahada na asiye na shahada wakati jina lake
limo kwenye Daftari la kupiga kura ipewe fursa hiyo.
Naye Bi. Amina Salum Ali aliwataka wananchi
wa Kaskaznini kutobabaishwa na maneno ya wapinzani huku akieleza miongoni mwa
mafanikio yaliopatikana katika Mkoa huo, ikiwa ni pamoja na uimarishwaji wa
miundombinu ya barabara pamoja na huduma nyengine za kijamii.
Aidha, aliendelea kueleza kufarajika
kwake na mipango ya Dk. Shein ya kuimarisha sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha Zanzibar inalima na kuzalisha mchele wake wenyewe.
Nae Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir ambaye pia ni mgombea
Uwakilisgi Jimbo la Tumbatu,alisema kuwa WanaCCM wanasubiri siku ya tarehe 25
Oktoba mwaka huu kukirejesha madarakani chama hicho.
Mapema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Kaskazini Unguja Haji Juma Haji, alisikitishwa na kauli za chama cha CUF
zinazoelezwa katika mikutano yao kuwa Zanzibar itaongozwa na wale walioondoshwa
mwaka 1964 pamoja na kuwahakikishia wananchi kuwa Serikali hiyo itaingia madarakani
na wale wote waliochukuliwa mashamba yao wanawarudishiwa mashamba yao kwani
yamechukuliwa kwa dhulma.
Alieleza kuwa wanaCCM wanaamini kuwa
uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa huru, haki na amani, na kusema kuwa vitendo vinavyofanywa
na CUF katika Mkoa huo hawaridhiki kwani wameanza kuchana picha za wagombea wa
CCM na kuwataka vijana wa Mkoa wa Kaskazini wasikubali kutumiwa na CUF kufanya
hivyo.
Alisisitiza kuwa Mkoa wa Kaskazini
ushindi hauna mbadala, huku akishangazwa wale wanaoparamia miti na kuanza
kuchana picha za wagombea wa CCM"Waanaparamia
miti kwaru kwaru utazani kima wanagombana na picha zisizosema waje kugombana na
mimi Haji Juma nnosema',alisema Haji.




No comments:
Post a Comment