TANGAZO


Wednesday, August 26, 2015

Watu 4 wahukumiwa kifo Saudi Arabia

Image copyright
Image captionMfumo wa sheria wakosolewa Saudia kutokana na ongezeko la hukumu ya kifo
Shirika la Amnesty International limeishtumu serikali ya Saudi Arabia kwa ongezeko la hukumu ya mauaji kama hayo na kusema kuwa mfumo wa sheria wa nchi hiyo una dosari.
Watu wote wanaopatikana na hatia ya mauaji, ujambazi ,ubakaji na uuzaji wa dawa za kulevya huhukumiwa kifo.
Imekuwa ni kawaida kushuhudia hukumu ya watu kukatwa vichwa Saudia.
Lakini kiwango cha visa hivyo kimekuwa kikiongezeka kwa wingi.
Image captionMaandamano yamefanyika kupinga hukumu hiyo ya kifo Saudia
Kiasi ya watu 130 wameuawa mpaka sasa mwaka huu- kiwango kilicho karibu mara mbili ya idadi mnamo 2013.
Haijulikani wazi lakini ghasia za kieneo huenda zinachangia ongezeko hilo la hukumu kali, na huku majaji zaidi wakiteuliwa huenda hukumu zaidi za aina hiyo zikatolewa.
Shirika la kimataifa la kutetea hakiza binaadamu, Amnesty International linasema mbinu zinazotumika kutoa hukumu ni pamoja na kuwatesa na kuwanyima washtakiwa haki ya kuwa na mawakili.
Visa kadhaa kama washtakiwa 7 wa wizi wa mabavu kukatwa vichwa -- wengi wao watoto walipokamatwa -- vimezusha wasiwasi hata ndani ya Saudi Arabia.

No comments:

Post a Comment