Wanafunzi wa darasa la sita wa Shule ya Msingi Kiburugwa ya Mbagala jijini Dar es Salaam,kutoka kushoto Mwajuma Abdallah, Khalima Khalfan na Mwanaid Mwakipesile wakimsikiliza kwa makini Ofisa Uhusiano na wateja wa benki ya KCB Tanzania, Victoria Kisima akiwafafanua jambo liloandikwa katika daftari wakati wa hafla fupi ya makabidhino ya msaada wa madawati 100 kwa shule hiyo.Benki hiyo inaendelea na kampeni yake ya kutoa msaada wa madawati 1000 kwa shule kumi za jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kiburugwa ya Mbagala jijini Dar es Salaam wakiwa wamekaa kwenye madawati 100 waliyopewa msaada na benki ya KCB Tanzania wakati wa hafla fupi ya makabidhino ya msaada wa madawati hayo kwa shule hiyo. Benki hiyo inaendelea na kampeni yake ya kutoa msaada wa madawati 1000 kwa shule kumi za jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kiburugwa ya Mbagala jijini Dar es Salaam wakibeba madawati kuyapeleka madarasani baada ya kukabidhiwa rasmi msaada wa madawati 100 na benki ya KCB Tanzania ikiwa ni sehemu ya mradi wa madawati 1000 kwa shule za msingi 10 za msingi jijini Dar es Salaam.





No comments:
Post a Comment