Newcastle United ilijitahidi nakuwadhibiti wenyeji wao Manchester United katika mechi ya kwanza ya ligi kuu ya Uingereza iliyomalizika muda mchache uliopita uwanjani Old Trafford.
Newcastle ilijifurukuta na kuvunja rekodi ya kushinda mechi zote msimu huu iliyokuwa imewekwa na Man united.
Chini ya mkufunzi Steve MClaren, Newcastle United ilikaza buti na kuwanyima washambuliaji wa manchester fursa ya kushambulia lango lao.
Aidha vijana hao wa Mclaren walijizolea alama yao ya pili msimu huu.

Vijana wa kocha Louis van Gaal hata hivyo walitamaushwa na kauli ya refarii aliyepuliza kipenga na kuashiria bao la mshambulizi Wayne Rooney kuwa halikufaa na kuwa alikuwa ameotea
Nusura Newcastle wafunge bao la kwanza kupitia mkwaju wa Aleksander Mitrovic uliogonga mwamba wa lango baada ya kuwapita walinzi na kipa wa manchester.
Mshambulizi huyo wa Serbia aliwaacha walinzi wa manchester hoi.
Muda mchache baadaye nipe nikupe kati ya washambulizi wa Manchester nusura izae matunda isipokuwa tu juhudi za Tim Krul wa Newcastle aliyezima kombora la Javier Hernandez.

Mashambulizi hayakuishia hapo, vijana wa van Gaal waliendelea kushambulia lango la Newcastle hadi dakika ya mwisho dakika tano za ziada Chris Smalling alipogonga mchuma wa
Newcastle sekunde chache tu kabla ya mechi hiyo kumalizika.
Man Utd 0 - 0 Newcastle
Mpira umekwisha
90:30 Muda wa kawaida umekwisha hapa Old Trafford na hakuna aliyeona lango la mwenziwe matokeo bado ni
Man Utd 0-0 Newcastle
88:30
Newcastle United.
Papiss Demba Cissé anachukua nafasi ya Aleksandar Mitrovic.
86:43
Man Utd 0 - 0 Newcastle
Free kick kuelekea lango la Man United
Jack Colback (Newcastle United)

85:13
Kona
Manchester United. Chancel Mbemba.
Man Utd 0 - 0 Newcastle
83:14
Man Utd 0 - 0 Newcastle
72:20

Juan Mata (Manchester United) anafyatua mkwaju lakini wapi !!!
68:57 Newcastle United.
Florian Thauvin anaingia kuchukua nafasi ya Gabriel Obertan.
66:56
Manchester United. Javier Hernández anachukua nafasi ya Adnan Januzaj.

Man Utd 0 - 0 Newcastle
65:09
Freekick kuelekea upande wa Manchester United
Chancel Mbemba (Newcastle United)
58:08
Manchester United. Michael Carrick anachukua nahfasi ya
Bastian Schweinsteiger.
57:39
Offside,Manchester United.
Chris Smalling amepatikana akiotea !
56:21
Man Utd 0 - 0 Newcastle

Gabriel Obertan (Newcastle United) anaoneshwa kadi ya njano
53:07
Free kick
Adnan Januzaj (Manchester United)
00:49
Kona kuelekea upande wa Manchester United
Man Utd 0 - 0 Newcastle
00:46
Man Utd 60 % -40%Newcastle Utd Kipindi cha pili kimeanza
00:45

Man Utd 60 % -40%Newcastle Utd
Kipindi cha kwanza kimekamilika matokeo bado ni sufuri bin sufuri
Kipindi cha kwanza kimekwisha.

Man Utd 0-0 Newcastle
00:40
Kona , Newcastle United. Sergio Romero
Man Utd 0 - 0 Newcastle
00:38 Offside
Luke Shaw amejenga kiota kwa ardhi ya wenyewe !
Man Utd 0 - 0 Newcastle
Mpira umesimamishwa Chris Smalling anacheza visivyo
00:35 Freekick kuelekea lango la Man Utd
Georginio Wijnaldum (Newcastle United
Man Utd 0 - 0 Newcastle
00:30

Offside Newcastle United. Aleksandar Mitrovic
Man Utd 0 - 0 Newcastle
00:28

Man Utd 0 - 0 Newcastle
Bastian Schweinsteiger anaonekana anachechemaa baada ya kugongana na Gabriel Obertan.
00:25

Man Utd 0 - 0 Newcastle
Wayne Rooney anapoteza nafasi nzuri
Aleksander Mitrovic anapoteza nafasi nzuri anagonga mchuma
Man Utd 0 - 0 Newcastle

Je Rooney atafanya mambo yake ?
Manchester United wanawakaribisha Newcastle katika uwanja wa nyumbani wa Old Trafford katika mechi hii ya mapema
00:15'

Man Utd 0 - 0 Newcastle 15''


No comments:
Post a Comment