TANGAZO


Friday, August 21, 2015

Rais Kikwete apokea hati za utamblisho wa Mabalozi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto), akipokea hati ya utambulisho ya Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kulia) leo Ikulu jijini Dar es salaam wakati alipokwenda kujitambulisha. 
Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen akisaini kitabu cha wageni wakati alipokuwa anaenda kukabidhi hati ya utambulisho na kujitambulisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete leo Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kulia) wakati alipokwenda kujitambulisha na kukabidhi hati ya utambulisho leo Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kulia) wakati alipokwenda kujitambulisha na kukabidhi hati ya utambulisho leo Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akisalimiana na Balozi wa Denmark (kushoto) nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen mara baada ya kukabidhi hati ya utambulisho leo Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akibadilishana mawazo na Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kushoto) wakati alipokwenda kujitambulisha na kukabidhi hati ya utambulisho leo Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akibadilishana mawazo na Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kushoto) wakati alipokwenda kujitambulisha na kukabidhi hati ya utambulisho leo Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Maadhi Juma Maalimu (wa pili kushoto) leo Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (katikati mstari wa mbele) akiwa amesimama wakati nyimbo za taifa za Tanzania na Denmark zikiimbwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokwenda kujitambulisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Bendi ya Jeshi la Polisi nchini ikipiga nyimbo za taifa za Tanzania na Denmark wakati Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (katikati mstari wa mbele) alipokuwa anakwenda kujitambulisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete. 
(Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)


Na Magreth Kinabo- MAELEZO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho wa Mabalozi wawili wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.

Utambulisho huo ulifanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam, ambapo Balozi wa kwanza  kuwakilisha hati ya utambulisho alikuwa ni Balozi wa India, Sandeep Arya na wa pili Balozi wa Denmark, Einer  Jensen.

Akizungumza na Balozi wa Denrmak Jensen, Rais Kikwete aliomba aendelee kuendeleza ,ushirikaino wa baina ya nchi hizo katika maeneo mbalimbali.

“Kwa sasa tunatoa kipaumbele katika uwekezaji wa kibiashara, kwa kuwa ni eneo ambalo tunaweza kutengeneza ajira mpya pia tunaweza kuwasaidia watu  kuweza kuondokana na umasikini,” alisema Rais.

 Rais Kikwete aliyataja baadhi ya maeneo   uwekezaji kuwa ni viwanda kutengenezea mbolea, madawa, na tunayo gesiasilia ya kutosha.

“Tunaweza kushirikiana katika maeneo mbalimbali. Hivyo hakuna kiongozi ambaye atakayeweza kusitisha ushirikiano wetu kwa kuwa ni agenda yetu hata nikiondoka madarakani,” alisisitiza Rais Kikwete.

Akizungumzia kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Rais Kikwete alisema mchakato wa kumtafuta mgombea kupitia Chama  Cha Mapinduzi(CCM)  na urudishaji fomu ulikwenda vizuri,  hivyo kampeni zitaanza wakati wowote kuanzia sasa.

Aliongeza kuwa ana matumaini kwamba kampeni za uchaguzi zitaendeshwa kwa usalama  kwa kuzingatia uhuru na haki.

Rais Kikwete alisema changamoto iliyopo katika harakati  za uchaguzi ni kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kupiga kura.

Kwa upande wake wa Balozi wa Denmark, Jensen, alisema  ana matumani kuwa mchakato wa uchaguzi  huo utamalizika kwa usalama.Pia ushirikiano wa baina ya nchi hizo utaendelea kuimarika.

No comments:

Post a Comment