TANGAZO


Thursday, August 20, 2015

Rais Jakaya Kikwete aagwa rasmi na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika sherehe ya kumuaga, Dar es Salaam leo, mara baada ya kumaliza uongozi wake katika Serikali ya Awamu ya Nne. (Picha zote na Anitha Jonas – MAELEZO.)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Tom Nyanduga katika Sherehe iliyoandaliwa na Tume ya kumuaga mara baada ya kumaliza Uongozi wake. 
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Tom Nyanduga akizungumza katika sherehe ya kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumaliza  utawala  wake katika serikali ya  awamu ya nne ,ndani ya  ofisi za tume hiyo. 
Baadhi ya viongozi wa Serikali pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi  wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika Sherehe ya kumuaga baada ya kumaliza uongozi wake katika serikali ya awamu ya nne. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora mara baada ya kuwasili katika ofisi yao, jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment