TANGAZO


Thursday, August 20, 2015

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia CCM Anthony Mavunde achukua fumo za kugombea nafasi hiyo

Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anthony Mavunde akizungumza na wanachama wa chama hicho pamoja na mashabiki wake mara baada ya kuchukua fomu za kuwania nafasui hiyo, mjini Dodoma jana. (Picha zote na John Banda)
Mavunde akionyesha Fomu hizo baada ya kuzichukua katika Ofisi za Manispaa jana.
Askari Polisi wakifuatilia msafara huo.  
Mavunde akionyesha Fomu hizo baada ya kuzichukua katika Ofisi za Manispaa jana.
Baadhi ya wafuasi wa Chadema wakionyesha ishara ya vidole viwili ambayo ni alama ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini wakati msafara wa Mgombea Ubunge Kupitia CCM Anthon Mavunde ulipokuwa ukipita kwenda kuchukua Fomu za kugombea nafasi hiyo, katika Barabara Kuu eneo la Nyerere Square. Hivi karibuni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma alikitaja kitendo hicho cha kuingiza itikadi ya chama kingine pasipohusika kama viashiria vya uvunjifu wa amani. 
Mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Dodoma Mjini  Anthon Mavunde akipokea Fomu za kugombea nafasi hiyo Toka kwa Ofisa Uchaguzi Manispaa ya Dodoma Elizabert Gumbo jana mjini Humo. 
Mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Dodoma Mjini, Anthon Mavunde akiwa katika msafara wakati akienda kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo. 
Mgombea Ubunge jimbo la Dodoma mjini kupitia CCM Anthon Mavunde akiwapungia watu mkono juu ya Gari wakati alipokuwa akienda kuchukua Fomu za kugombea nafasi hiyo. 
Msafara wa pikipiki ukimsindikiza Mavunde mara baada ya kuchukua fomu hizo.

No comments:

Post a Comment