TANGAZO


Wednesday, August 26, 2015

Beijing:Wakenya washinda dhahabu nyengine 2



Image captionHyvin Jepkemoi

Kenya imeshinda dhahabu nyengine mbili katika mashindano ya riadha yanayoendelea mjini Beijing Uchina baada ya mrusha mkuki Julius Yego na Hyvin Jepkemoi wa mita 3000 kuruka viunzi upande wa wanawake kuchukua dhahabu.
Mrusha mkuki wa Kenya Julius Yego alirusha umbali wa 99.72 na kushinda mchezo huo mbele ya aliyekuwa bingwa wa Afrika Abdelrahman el sayid wa Misri.


Image captionyego

Ni urefu ambao haujawahi kufikishwa duniani tangu Jan Zelezny ambaye anayeshikilia rekodi ya 98.48 katika mashindano ya dunia mwaka 2001.
Ni yeye na Aki Parviainen wa Finland waliorusha zaidi ya Yego.
Aliyekuwa bingwa wa mchezo huo barani Afrika Ihab Abdelrahman El Sayed wa Misri alijipatia medali ya fedha kwa kurusha umbali wa 88.99.


Image captionyego

Wakati huohuo Mkenya mwengine alikabili ushindani mkubwa kutoka kwa wanariadha wengine na kuweza kushinda mbio za mita 3000 kwa kumpita mwanariadha wa Tunisia habiba Ghribi ikiwa imesalia mita 30.
Mjerumani Gesa Krause alipata medali ya shaba baada ya kumaliza wa tatu huku bingwa wa Olimpiki na mshindi wa medali ya shaba Sofia Assefa wa Ethiopia akichukua nafasi ya nne.


Image captionyego

Kenya sasa imeshinda dhahabu zote mbili katika mbio za mita 3000 upande wa wanaume na wanawake baada ya Ezekiel Kembi kushinda dhahabu siku ya jumanne.

No comments:

Post a Comment