TANGAZO


Wednesday, July 15, 2015

Timu ya watu 39 wapanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha za kusaidia kununua vitambaa maalum vya wasichana

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa, Allan Kijazi (wasita toka kushoto waliosimama), akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya watu 39 wakiwemo Wakurugenzi wa kampuni ya Vodacom na kampuni mbalimbali za nchini Afrika Kusini kabla ya kuanza zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kununua vitambaa maalumu(Pedi) vya kuwahifadhi wasichana walioko mashuleni wakati wa hedhi. 
Ofisa Mkuu wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom, Afrika Kusini, Maya Makanjee (wapili toka kushoto), akiwa katika lango la kuanzia safari ya kupanda mlima Kilimanjaro, Makanjee anapanda mlima huo ikiwa ni sehemu ya changamoto ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kununua vitambaa maalumu kwa wasichana walioko mashuleni kujisitiri wakati wakiwa kwenye Hedhi.
Ofisa Mkuu wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom, Afrika Kusini, Maya Makanjee (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mratibu wa zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua vitambaa maalumu kwa wasichana walioko mashuleni kujisitiri wakati wakiwa kwenye Hedhi,Richard Mabaso (wa kwanza toka kushoto aliyeshika bendera), wengine ni washiriki wa zoezi hilo la kupanda Mlima Kilimanjaro kutoka Mataifa mbalimbali.  

Ofisa Mkuu wa Uhusiano wa Nje wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom, Afrika Kusini, Maya Makanjee akianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro akiwa ni miongoni mwa timu ya watu 39 waliopanda kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia fedha za kununua vitambaa maalumu kwa wasichana walioko mashuleni kujisitiri wakati wa hedhi. 
Ofisa Mkuu wa Uhusiano wa Nje wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom, Afrika Kusini, Maya Makanjee akianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.(Picha zote na Mpigapicha wetu)

No comments:

Post a Comment