TANGAZO


Friday, July 3, 2015

Simba, Tigo zazindua huduma ya Simba News jijini Dar es Salaam

Msemaji wa Timu ya Simba, Haji Manara, akizungumza wakati akimkaribisha Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva (wapili kulia), kuzungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, katika uzinduzi wa huduma ya Simba News kupitia Simu za mkononi za Tigo, ambapo mteja atajiunga kwa kuandika neno SIMBA kwenda namba 15460, kisha kukatwa sh. 150 kwa siku. Wapili kushoto ni Ofisa Mtendaji wa EAG group, Imani Kajula na kulia ni Meneja Mawasiliano ya Kibiashara wa Tigo, Jacqueline Nnunduma. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo ya Simba News kupitia Simu za mkononi za Tigo, ambapo mteja atajiunga kwa kuandika neno SIMBA kwenda namba 15460, na kisha kukatwa sh. 150 kwa siku. Kushoto ni Ofisa Mtendaji wa EAG group, Imani Kajula na kulia ni Meneja Mawasiliano ya Kibiashara wa Tigo, Jacqueline Nnunduma.
Meneja Mawasiliano ya Kibiashara wa Tigo, Jacqueline Nnunduma, akizungumza wakati wa mkutano huo. katikati ni Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na kushoto ni Ofisa Mtendaji wa EAG group, Imani Kajula.
Meneja Mawasiliano ya Kibiashara wa Tigo, Jacqueline Nnunduma, akizungumza wakati wa mkutano huo. katikati ni Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na kushoto ni Ofisa Mtendaji wa EAG group, Imani Kajula.
Ofisa Mtendaji wa EAG group, Imani Kajula, akizungumza katika mkutano huo. Katikati ni Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na kulia ni Meneja Mawasiliano ya Kibiashara wa Tigo, Jacqueline Nnunduma. 
Ofisa Mtendaji wa EAG group, Imani Kajula, akizungumza katika mkutano huo. Katikati ni Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na kulia ni Meneja Mawasiliano ya Kibiashara wa Tigo, Jacqueline Nnunduma.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, alipokuwa akijibu maswali yao na kufafanua mambo mbalimbali kuhusu huduma hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, alipokuwa akijibu maswali yao na kufafanua mambo mbalimbali kuhusu huduma hiyo.
Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa huduma ya Simba News kupitia Simu za mkononi za Tigo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji wa EAG group, Imani Kajula na kulia ni Meneja Mawasiliano ya Kibiashara wa Tigo, Jacqueline Nnunduma.

Na Stella Kessy
KAMPUNI ya tigo kwa kushirikiana na Klabu ya Simba wamezindua huduma ya ujumbe mfupiinayojulikana kama "Simba SMS",ambayo lengo ni kuwapatia wateja wa Tigo taarifa zinazohusu klabu ya Simba popote.

Akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo, Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva alisema, wana amini ubunifu huo bila shaka utawawezesha mashabiki wote wa Simba na wa soka kwa ujumla ambao pia ni wateja wa Tigo kupata habari mbalimbali za klabu ya Simba kupitia simu zao za mkononi.

Aveva alihimiza mashabiki wao wajiunge katika huduma hiyo, ili kupata na kufurahia habari.

"Tunawahimiza mashabiki wetu kujiunga na huduma hii kupitia Tigo ili waweze kupata nakufurahia habari mbalimbali kutoka klabu ya Simba"alisema Aveva.

Naye Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya EAG Group Ltd, Imani Kajula ambao ni washauri na  watekelezaji wa  shughuli za kibiashara na masoko katika klabu ya Simba.

“Tunatarajia kuendelea kuwapatia mashabiki wa Simba huduma za kisasa kwa kutumia teknolojia zisizokuwa na usumbufu wa aina yeyote kupitia wadau wanaoaminika ndani ya Tanzania”

Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile Solutions, Bi Lulu Ramole alisema kuwa huduma hii imetengenezwa ili kuwawezesha wateja kupata habari za papo kwa papo naaliongeza kuwa huduma ipo katika mfumo wa vifurushi vya Combo BUNDLE PACK ambapo wateja wa Tigo watakuwa wakilipia mara moja kwa siku na kupokea kiwango cha chini cha habari nne (04) na habari mpya za kila siku zina zohusu klabu ya Simba.

Huduma pia itamruhusu mteja aliyejiunga kujitoa kwenye huduma hii wakati wowote akitaka bila vikwazo vyovyote na pia kwenye huduma hii kutakuwepo na neon kuu 
“kwa ajili ya kusaidia juu ya maswali mbalimbali ya nayo ulizwa mara kwa mara na wateja wakati wakifurahia huduma.

Naye Meneja wa mawasiliano ya kibiashara Jackline Nnunduma alisema kuwa Lengo ni kuwapatia  wateja taarifa kiurahisi zaidi na kuwapatia taarifa kwa wakati na zenye uhakika kutoka katika vyanzo vya michezo vyenye kuaminika.

Pia alisema kuwa huduma hii ni kwa simu ya aina yoyote na mteja hatakuwa anakatwa 150 kwa huduma hii na kupata SMS 4 kila siku jinsi ya kujiunga ni neno Simba kwenda namba 15,460. 

No comments:

Post a Comment