Ofisa Mkuu Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Injia Peter Ulanga akibadilishana hati za makubaliano na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia mara baada ya kusaini mkataba wa kupeleka mawasiliano ya simu vijijini, katika sherehe zilizofanyika mjini Dodoma leo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Prof. Makame Mbarawa (katikati) akiwa na Wawakilishi wa makampuni ya simu yaliyosaini mkataba wa kupeleka mawasiliano ya simu vijijini sherehe iliyofanyika mjini Dodoma leo. Wengine ni Mwakilishi wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano, Aumsuri Moshi (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano Injinia Peter Ulanga. Mstari wa nyuma ni wawakilishi wa makampuni hayo ya simu, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura, Mwakilishi wa Vodacom Tanzania, Rosaline Mworia na Mwakilishi wa MIC Tanzania Ltd, Sylivia Balwire.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Prof Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akiwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia mara baada ya kampuni ya Vodacom kuwa kati ya makampuni matatu yaliyosaini mkataba wa kupeleka huduma ya mawasiliano simu vijijini awamu ya 2B katika sherehe zilizofanyika mjini Dodoma leo.
No comments:
Post a Comment