TANGAZO


Monday, May 18, 2015

Rais Filipe Nyusi aahidi kushirikiana na Tanzania kukiendeleza Chuo cha Diplomasia

Rais Jakaya Kikwete akiwapungia wananchi, waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam jana, kumpokea mgeni wake, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi (kushoto), mara alipowasili uwanjani hapo.
Rais Jakaya Kikwete (kulia), akiwa na mgeni wake, Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam jana.

Na Magreth Kinabo – Maelezo
RAIS wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi ameahidi kuendeleza ushirikiano wa pamoja  katika kukuza na kukiendeleza Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam ili kuweze kuwa chuo chenye kiwango cha juu  cha Kimataifa.

Kauli hiyo  ilitolewa leo na Rais Nyusi wakati alipotembelea chuo hicho, ambapo alisema katika mazungumzo yake na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe .Dkt . Jakaya Mrisho Kikwete wamezungumzia jinsi ya kukiimarisha ili kiweze kuwa kumbukumbu ya wapigania uhuru si kwa nchi hizo bali hata kwa nchi za Kusini wa Afrika.

“Mimi  na Rais Kikwete katika mazunguzo yetu  ya jana , tumezungumzia jinsi ya kuendeleza kituo hiki .” alisema Rais Nyusi.
Aidha Rais Nyusi aliahidi kutoa nafasi ya kubadilishana uzoefu katika mafunzo kupitia ushirikiano huo, ambapo wanafunzi wa chuo hicho na wakufunzi watakuwa wanakwenda Msumbiji.

Aidha  Rais Nyusi aliwataka wanafunzi wa chuo hicho, kujiandaa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza  katika serikalini na   sekta binafsi wakiwa wanadiplomasia  badala ya kutegemea kuwa mabalozi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo hicho, Balozi Mwanahidi Majaar alisema  wanampango wa kukiboresha chuo hicho ili kiweze kuwa chuo bora cha kimataifa katika nchi zilizo Kusini mwa Afrika.

No comments:

Post a Comment