Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania Grace Lyon, akiwasikiliza jambo baadhi ya watoto waliofika na wazazi wao katika maadhimisho ya Kimataifa yaliyofanyika kitaifa katika Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita. Vodacom Foundation ilikabidhi Hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100/- Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Kassim Majaliwa (hayupo pichani) kwa niaba ya Hospitali ya CCRBT kwa ajili ya kutokomeza fistula nchini, Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka Mei 23.
Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCRBT Haika Mawala (kushoto) na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon wakimuangalia mtoto Nyambole Kulubone mwenye tatizo la mdomo wa sungura akiwa amebebwa na mama yake Mariam Sanda(22) Mzazi huyo aliyehudhuria katika Maadhimisho ya Kimataifa ya Fistula aliaidiwa na Mkurugenzi wa hospitali ya CCBRT(kushoto) kuwa mtoto huyo atatibiwa bure katika hospitali hiyo wakati walipomuona kwenye Maadhimisho ya Kimataifa ya Fistula yaliyofanyika kitaifa katika Wilaya Mbogwe Geita. Ambapo Taasisi ya Vodacom Foundation ilimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 100/-Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Kassim Majaliwa (hayupo pichani) kwa niaba ya Hospitali hiyo kwa ajili ya kutokomeza fistula nchini, Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka Mei 23.
Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Kassim Majaliwa (kushoto) akimsisitiza jambo Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Grace Lyon, wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Fistula yaliyofanyika kitaifa katika Wilaya Mbogwe Geita.Meneja huyo alimkabidhi waziri huyo hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 100/- iliyotolewa na taasisisi ya Vodacom foundation kwa ajili ya kutokomeza fistula nchini.
Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Grace Lyon(kushoto) akimsisitizi jambo Balozi wa Fistula nchini Mrisho Mpoto wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Fistula yaliyofanyika kitaifa katika Wilaya Mbogwe Geita mwishoni mwa wiki. Ambapo Taasisi ya Vodacom Foundation ilimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 100/- Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Kassim Majaliwa(hayupo pichani)kwa niaba ya Hospitali ya CCBRT kwa ajili ya kutokomeza fistula nchini, Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka Mei 23.






No comments:
Post a Comment