TANGAZO


Saturday, April 18, 2015

Zaidi ya 74% ya wanandoa wamepata elimu ya afya ya uzazi na jinsia

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Digital Opportunity Trust Bw. Eliguard Dawson akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Mbagala Zakheem uliopo wilayani Temeke leo wakati wa tamasha la Jamvi la Vijana lililoandaliwa na  Kituo cha Vijana cha UMATI –Temeke. 
Afisa Vijana wa Kituo cha Vijana UMATI –Temeke jijini Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati  wa tamasha la Jamvi la Vijana lililoandaliwa na  Kituo hicho na kufanyika katika Mtaa wa Mbagala Zakheem uliopo wilayani Temeke leo 
Baadhi ya Vijana wakifuatilia maigizo kutoka kwa makundi mbalimbali ya vijana yaliyokuwa yakutoa elimu ya kuhusu afya ya uzazi na jinsia kwa nija ya sanaa ya maigizo wakati wa tamasha la Jamvi la Vijana lililoandaliwa na  Kituo cha Vijana cha UMATI –Temeke leo 
Kikundi cha sanaa kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe wakiigiza kuhusu matumizi ya njia za uzazi wa mpango wakati wa tamasha la Jamvi la Vijana lililoandaliwa na  Kituo cha Vijana cha UMATI –Temeke na kufanyika katika mtaa wa Mbagala Zakheem leo 
Kikundi cha sanaa kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe wakiigiza kuhusu matumizi ya njia za uzazi wa mpango wakati wa tamasha la Jamvi la Vijana lililoandaliwa na  Kituo cha Vijana cha UMATI –Temeke na kufanyika katika mtaa wa Mbagala Zakheem leo 
Kikundi cha sanaa kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe wakiigiza kuhusu matumizi ya njia za uzazi wa mpango wakati wa tamasha la Jamvi la Vijana lililoandaliwa na  Kituo cha Vijana cha UMATI –Temeke na kufanyika katika mtaa wa Mbagala Zakheem leo.
Kikundi cha sanaa cha Ndio Sisi Group wakiigiza kuhusu matumizi ya njia za uzazi wa mpango wakati wa tamasha la Jamvi la Vijana lililoandaliwa na  Kituo cha Vijana cha UMATI –Temeke na kufanyika katika mtaa wa Mbagala Zakheem leo. 
Kikundi cha sanaa cha Ndio Sisi Group wakiigiza kuhusu matumizi ya njia za uzazi wa mpango wakati wa tamasha la Jamvi la Vijana lililoandaliwa na  Kituo cha Vijana cha UMATI –Temeke na kufanyika katika mtaa wa Mbagala Zakheem leo. 
Mmoja wa vijana waliohudhuria Jamvi la vijana lililoandaliwa na  Kituo cha Vijana cha UMATI –Temeke na kufanyika katika mtaa wa Mbagala Zakheem akipata huduma ya ushauri nasaha ambayo ilikuwa ikitolewa bure wakati wa tamasha hilo leo. (Picha zote na Frank Shija, WHVUM)

Na Frank Shija, WHVUM
ZAIDI ya asilimia 74 ya watu walio kwenye ndoa wamepata elimu ya Afya ya Uzazi na Jinsia nchini Tanzania.
Haya yamebanishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Digital Opportunity Trust ya jijini Dar es Salaam Eliguard Dawson alipokuwa mgeni rasmi wakati wa tamasha la Jamvi la Vijana lililofanyika leo jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Mbagala Zakhem.

Dawson alisema kuwa elimu kuhusu afya ya uzazi imekuwa ikitolewa toka enzi za mababu zetu ambapo wanaume walikuwa wanapelekwa jandoni wakati wanawake wanaenda unyagoni ambapo elimu mbalimbali kuhusu makuzi zilitolewa kwa vijana.

“Suala hili la elimu kuhusu afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana si jambo geni kwani limekuwa likitolewa toka enzi za mababu zetu”. Alisema Dawson.

Kwa upande wake Afisa Vijana wa Kituo cha Vijana UMATI kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam Bi. Upendo Daud alisema kuwa pamoja na nia njema ya UMATI kutoa bure elimu ya afya ya uzazi na jinsia kwa vijana lakini wamekuwa wakikumbana na changamaoto kadhaa.

Ametaja kuwa changamoto kubwa wanayo kumbana na nayo ni wazazi wengi kupokea elimu hiyo kwa hisia hasi jambo ambalo linawapa wakati mgumu wa kufikia malengo yao ambayo ni kufikia idadi ya vijana 200 katika kila Jamvi la Vijana wanaloendesha.

Upendo ameongeza kuwa pamoja na changamoto hizo wamekuwa wakifanya jitihada za makusudi ili kuhakikisha wazazi nao wanapata hamasa kuhusu elimu hiyo na hatimaye kutoa fursa kwa vijana wao wawezekushiriki vyema katika kupata elimu juu ya afya ya azazi na jinsia.


UMATI kupitia kituo chake cha vijana cha Temeke jijini Dar es Salaam wamekuwa wakiandaa na kuendesha mtamasha ya vijana yaliyopewa jina la Jamvi la Vijana ambayo huwa na kauli mbiu mbalimbali ambapo katika Jamvi la mwezi huu ni “Elimu ya afya ya uzazi na jinsia kwa vijana inajenga au ina moboma maadili?”

No comments:

Post a Comment