TANGAZO


Sunday, April 19, 2015

Waziri wa Fedha Saada Mkuya na ujumbe wake akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Afrika, Uongozi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia

Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati  akiandika maelezo na hoja kutoka Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la Afrika (Afrika Group 1 Constituency), Bi. Chileshe Mpundu Kapwepwe (hayupo kwenye picha). kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile na kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa na akifuatiwa  na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania  Bi. Natu Mwamba.
Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati  akiwa pamoja na ujumbe  kutoka Tanzania katika majadiliano na Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la Afrika ( Afrikca Group 1 Constituency)Bi. Chileshe Mpundu Kapwepwe(hayupo kwenye picha). kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile akifuatiwa na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa na kufuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania  Bi. Natu Mwamba.Pamoja na ujumbe kutoka Tanzania.
Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya akielezea jinsi Tanzania inavyotekeleza sera zilizowekwa na mashirika ya kimataifa kama (WB) na (IMF) kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency), Bi. Chileshe Mpundu Kapwepwe. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile.

Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya akisikiliza kwa makini maswali aliyokuwa akiulizwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency), Bi. Chileshe Mpundu Kapwepwe hayupo kwenye picha. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile.
Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati  akiwa pamoja na ujumbe  kutoka Tanzania walipokutana na uongozi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile na Bw. Ngosha Saidi Magonya, Kamishna wa Fedha za nje.Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani – Washington Mhe.Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Wizara ya fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa na Bw. Laston Msongole ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa milenia wa awamu ya pili. 
Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya (katikati) akisikiliza kwa makini maelezo na msimamo wa uongozi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) hawapokwenye picha. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dr. Servacius Likwelile na kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani – Washington DC. Mhe. Liberata Mulamula. 
Makamu wa Rais wa shughuli za operesheni  za mfuko wa Changamoto za Milenia, Bw. Kamran Khan (katikati), akitoa maelezo na msimamo wa mfuko wa Changamoto za milenia. Wengine ni viongozi wa mfuko wa changamoto za Milenia wakiongea na ujumbe wa Tanzania (hawapo kwenye picha).

Makamu wa Rais wa shughuli za operesheni  za mfuko wa Changamoto za Milenia, Bw. Kamran Khan akizungumza na ujumbe kutoka Tanzania na kutoa maelekezo ya jinsi ya kuutumia mfuko huo nchini Tanzania.
Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati, akiwa pamoja na ujumbe  kutoka Tanzania walipokutana na uongozi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) hawapo kwenye picha. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile na Bw. Ngosha Saidi Magonya, Kamishna wa Fedha za nje. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani – Washington Mhe. Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Wizara ya fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa. (Picha zote na Ingiahedi  Mduma- Washington DC.)

No comments:

Post a Comment