Baadhi ya wajummbe kutoka nchini Korea ya Kusini wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati alipokuwa fungua kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu.
Baadhi ya wajummbe kutoka Tanzania wakifuatilia mjadala wakati wa kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu.
Picha ya pamoja ya
wajumbe kutoka Tanzania na Korea ya Kusini walioshiriki kongamano la siku moja lililofanyika
leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji ili kubadilishana uzoefu
na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta
ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu. Kutoka kushoto
walioketi ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda. (Picha na Wizara ya
Fedha)
Na mwandishi wetu.
SERIKALI ya Tanzania na
Korea ya Kusini zimefanya kongamano la siku moja kuhusu masuala ya kiuchumi ili
kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili
kwa kushirikisha sekta ya Umma pamoja na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo
endelevu.
Kauli hiyo imetolewa
leo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda alipokuwa akifungua
kongamano hilo lililofanyika leo jijini Dar es salaam.
Kongamano hilo lilikuwa
na lengo kuiwezesha Tanzania kujifunza namna ya kuendesha masuala ya bajeti ya
nchi na namna ya kushirikisha sekta binafsi na sekta ya Umma katika kuinua
uchumi wa nchi.
Prof. Adolf Mkenda
alisema kuwa kupitia kongamano hilo Tanzania imejifunza kutoka Korea ya Kusini
namna ya kushirikisha sekta binafsi na sekta ya Umma katika kuwaletea wananchi
maendeleo endelevu na ya nchi kwa ujumla.
“Kama nchi, tumeona ni
vema kujifunza kutoka kwa wenzetu wa Korea ya Kusini ili kupata fursa na uzoefu
katika kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuwa Korea ya Kusini ni miongoni mwa
nchi zinzoongoza duniani kwa kuwa na uchumi imara walionao kwa kushirikisha
sekta binafsi” alisema Prof. Mkenda.
Ili kupata maendeleo
endelevu, Prof. Mkenda alisema kuwa jukumu la Serikali ni kushirikiana na sekta
binafsi na kujiwekea mikakati mbalimbli itakayosaidia kuibua miradi ambayo
itakuwa na ushindani ambapo kwa namna hiyo itasaidia nchi kuwa na maendeleo na
hivyo kupata faida na kuinua uchumi wa nchi na kuongeza kipato cha mtu mmoja
mmoja na taifa kwa ujumla.
Aidha, Prof. Mkenda
alisema kuwa fursa hiyo ya kushirikisha sekta binafsi imeanza kuwa na mafanikio
nchini ambapo tayari Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepisha mswada
wa namna ya Serikali kushirikiana na sekta binafsi (PPP) katika kuleta
maendeleo nchini.
Kwa upande wake
mwakilishi wa Korea ya Kusini Dkt. Cae One Kim aliishukuru Serikali ya Tanzania
kwa kuwa na ushirikiano mzuri katika kukuza na kuinua uchumi kati ya nchi hizo mbili
ambapo Serikali zote mbili zinaimarisha na kujenga ushirikiano na sekta binafsi
katika kujiletea maendeleo.
Dkt. Kim alisema kuwa
uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya pande hizo mbili ndiyo umekuwa ni msingi
wenye manufaa ambapo utaendelea kukuza sekta za kiuchumi, kibiashara,
teknolojia na masuala ya kiutamaduni kati ya nchi hizo.
“Serikali ya Korea imetambua
na kuiona Tanzania ni sehemu muhimu katika kukuza mahusiano ya kiuchumi ambayo
yatasidia nchi hizi mbili kunufaika, kukuza na kuimarisha uhusiano uliopo baina
yetu” alisema Dkt. Kim.
Mahusiano ya
kidiplomasia kati ya Tanzania na Korea ya Kusini siyo ya muda mrefu kama ilivyo
kwa Korea ya Kaskazini.
Uhusiano huo kihistoria
umeanza katika miaka ya 1990 ambapo Korea ya Kusini imekuwa nchi ya matumaini
kwa kuwa imepata maendeleo makubwa duniani ambapo Tanzania itaendelea kunufaika
na kujifunza ili kuimarisha uchumi wake hasa katika kipindi hiki cha ushindani
katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
No comments:
Post a Comment