Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius
Likwelile kushoto kwake kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa
kisheria wa kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea
mjini Washington DC.
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na
Katibu Mkuu wa kwa pamoja wakifuatilia kwa makini
mkutano wa 10 wa
kisheria kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini
Washington DC.
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius
Likwelile kushoto kwake kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa kisheria wa kundi la
Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius
Likwelile kushoto kwake kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa
kisheria wa kundi la Afrika (Afrikca
Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha
Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu
wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto kwake kwa pamoja
wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa kisheria wa kundi la Afrika (Afrikca
Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto wakifuatilia
semina iliyokuwa ikitolewa kuhusu uimarishaji wa makazi mijini.
Waziri wa Fedha
Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu
wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto wakifuatilia semina
iliyokuwa ikitolewa kuhusu uimarishaji wa makazi mijini. Aliyeko nyuma ya
waziri ni Bw. Ngosha Saidi Magonya, Kamishina wa Fedha za nje.
NCHI ZA AFRIKA
ZA TOA MSIMAMO WAO KWA IMF NA WB
WAKATI Mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la kifedha la kimataifa ikiendelea hapa Mjini
Washington Dc. Mawaziri wa fedha wameweka misimamo yao juu ya sera ambazo
zinawekwa na Benki ya Dunia.
Akizungumza
na vyombo vya habari,waziri wa fedha wa
Tanzania Mhe. Saada Salum Mkuya alisema” Sisi kama nchi tuliwasilisha nini tunaona katika
utekelezaji wa mipango ya Benki. Tumeshukuru sana Benki ya Dunia kwa kuendeleza
mipango ya kuweza kusaidia nchi za kiafrika ,hususan kwenye mipango ya kujenga miundo mbinu ya kiuchumi kama vile barabara, kilimo pamoja na miundo
mbinu ya maji na umeme”.
“Lakini
vilevile tumeonyesha wasiwasi wetu kutokana na sera ambazo Benki ya Dunia
imeziweka, kama vile kuangalia sera zile za watu wa kiasili ya kiafrika, sisi tumehisi
mbali ya nia nzuri na njema ya Benki hii ya Dunia, lakini inaweza kuwa ni
kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi zetu
kwa sababu sera hiyo inaweza kutumika kuigawa nchi ambayo misingi yake
imekuwa ikijengwa kwa umoja kutoka uhuru”.Alisistiza Mkuya.
Hakuishia
hapo aliendelea kutoa mfano kuwa “sisi watanzania tumekuwa wamoja ingawa tuna lugha
mbalimbali kutokana na makabila tofauti. Lakini tumekuwa pamoja kwa kipindi cha
miaka 50.Kwa hiyo tumeona sera hiyo isije ikatumika kwa ajili ya kuwa kigezo
cha utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.
Sisi kama wa Afrika na viongozi
wa Afrika tunashirikiana kuona kuwa sera zinazowekwa hazitukwamishi”.
Hali
hii ya kudai uasilia (indigenous) imeibuka
zaidi katika miongo hii miwili, wakati kukiwa kumejitokeza watu wanaodai kuwa
wao hawatambuliki na hoja hii inaihusu
hasa nchi ya Tanzania.
Mawaziri
wa Fedha kutoka Afrika wamejadili mambo mbali mbali ambapo ni pamoja na masuala
ya maendeleo na mahusiano yao na Benki
ya Dunia.
Katika
Mkutano huo wa kisheria Mkurugenzi
Mtendaji ndiye ambaye amewasilisha maazimio ya Benki katika kipindi cha miezi sita.Aliongeza Mkuya.
Aidha
katika mkutano huo pia walizungimzia suala la Ebola. “Kwa kweli wamekubali
kusaidia nchi zile ambazo zimekumbwa na gonjwa hili lakini wamezitaka nchi za
afrika na zenyewe kushirikiana katika kupambana na gonjwa hili”.Alimalizia
Mkuya.
Mikutano
hiyo bado inaendelea hapa mjini Washington DC. Hali ya hewa ni baridi kiasi.
Imetolewa na Msemaji :Wizara ya fedha
Ingiahedi C.Mduma
Washington DC
18/04/2015

No comments:
Post a Comment