Kocha wa kilabu ya Borrusia Dortmund Jurgen Klopp amesema ataondoka katika kilabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Mkufunzi huyo wa miaka 47 kutoka Ujerumani alitaka asimamishiwe kandarasi yake ambayo ilitarajiwa kukamilika mwaka 2018.
''Sio kwamba nimechoka,sijakuwa na mawasiliano na kilabu yoyote,lakini sina mpango wa kuchukua likizo''.alisema.

Klopp ameifunza Dortmund tangu mwaka 2008,na kuwasaidia kushinda mataji mawili ya ligi mbali na kucheza katika fainali za kombe la kibalu bingwa ulaya mwaka 2012-13,lakini sasa wako katika nafasi 10.
Kwa sasa wako pointi 37 nyuma ya viongozi wa ligi ya Ujerumani Bayern Munich.
Klopp ameuambia mkutano na waandishi wa habari:'' nilikuwa nikisema kwamba ninaamini mimi sio mkufunzi mzuri zaidi katika kilabu hii''.


No comments:
Post a Comment