Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia inatarajiwa kuwasili Dar es Salaam wiki hii kwa ajili ya mechi yao ya kukata na shoka dhidi ya Yanga katika kombe la vilabu la Shirikisho barani Afrika.
Habari kutoka Yanga zinasema wapinzani wao wanaweza kutinga Dar es Salaam kati ya Alhamisi au Ijumaa kwa mechi ya kwanza itakayochezwa kati ya April 17 au 18 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi ya marudiano itachezwa Tunis, Tunisia baada ya wiki mbili.
Yaanza imeanza kuwavutia kasi wapinzani wao kufuatia wimbi la ushindi katika mechi zake za Ligi kuu.
Katika mechi za hivi karibuni, mabingwa hao wa zamani waliweka historia ya mvua ya magoli katika msimu baada kwa kuipa Coastal Union kichapo cha 8-0 na baadae Mbeya City 3-1 na kujikita kileleni ikiwa name pointi 46.
Tayari kocha wa Yanga, Hans Pluijm amewaonya wachezaji wake kuwa makini na kuweka akilini kuwa watakutana na moja ya timu ngumu barani Afrika katika hatua ya 16 bora .
Yanga iliwatoa Wazimbabwe, Platinum FC na sasa itatumia mechi zake za ligi kuu kama sehemu ya mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo muhimu.
No comments:
Post a Comment