TANGAZO


Wednesday, April 1, 2015

AU yapongeza uchaguzi Nigeria

Mkuu wa Umoja wa Afrika Nkosana Dlamini Zuma
Mkuu wa umoja wa Afrika ,Nkosana Dlamini Zuma anasema kuwa uchaguzi wa Muhammadu Buhari kama rais mpya wa Nigeria unaonyesha ukuwaji wa demokrasi nchini Nigeria.
Rais anayeondoka Goodluck Jonathan ambaye alishindwa kwa kura millioni mbili alimpigia bwana Buhari siku ya jumanne ili kukubali kushindwa.
Msemaji wa bwana Jonathan amesema kuwa alikuwa na furaha licha ya kupoteza uchaguzi huo.
Bwana Buhari hatochukua mamlaka hadi mwisho wa mwezi Mei na atachukua mda wa wiki chache zijazo kujenga serikali yake.
Kiongozi huyo wa zamani wa jeshi alifanya kampeni ya mwana demokrasia anayetaka kusafisha siasa za taifa hilo.

No comments:

Post a Comment