TANGAZO


Sunday, March 15, 2015

Watanzania waombwa kumpigia kura Mayunga awe mshindi wa Airtel Trace Africa

*Msanii maarufu Akon kuwa mgeni wa heshima mashindano Fainali za Airtel Trace Nairobi
Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Bi. Aneth Muga akiongea na waandishi wa habari na kuwasikilizisha nyimbo hii chipukizi  kwa lengo la kuwafikishia ujumbe wapenda burudani na Watanzania kwa ujumla kumpigia kura msanii chipukizi huyo ambae ni mshindi wa Airtel Trace Music Stars wa Tanzania Nalimi Mayunga (wakwanza kulia) ili arudishe
ushindi nchini atakapoiwakilisha Tanzania katika fainali za aAfrika za Airtel Trace Music Stars Nairobi machi, 28 2015 katika hotel maarufu ya Enashipai iliyopo jijini humo (kati ni Meneja uhusiano wa Airtel 
Bw. Jackson Mmbando. 

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mmbando
akiongea na waandishi wa habari leo ili kumuombea mshindi wa Tanzania wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga (wakwanza kulia), apigiwe kura ili kushinda fainali za shindano hilo la Afrika litakaloshindanisha wasanii toka nchi 13 Afrika huko Nairobi. Kumpigia kura mayunga andika YUN kwenda 15594, wakwanza kushoto ni Meneja masoko wa Airtel Bi Aneth 
Muga. 
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mmbandoakiongea na waandishi wa habari leo, ili kumuombea mshindi wa Tanzania wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga (wakwanza kulia), apigiwe kura ili kushinda fainali za shindano hilo la Afrika litakaloshindanisha wasanii toka nchi 13 Afrika huko Nairobi. Kumpigia kura mayunga andika YUN kwenda 15594. Wakwanza kushoto ni Meneja masoko wa Airtel Bi Aneth Muga.  
Msanii chipukizi na mshindi wa Airtel Trace Music stars Tanzania Nalimi Mayunga (wakwanza kulia) akiimba kwa ushawishi, wakati wa mkutano na wanahabari leo, akiomba kura kwa watanzania ili ashide fainali za Afrika za Airtel Trace Music Stars zinazotarajiwa kufanyika Nairobi Kenya kwenye Hotel ya Eneshipai tare machi 28. Katikati ni Meneja Uhushiano wa Airtel, Jackson Mmbando na kushoto ni Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga katika makao makuu ya Airtel Tanzania.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imetoa wito kwa watanzania na wapenda burudani kwa ujumla kumpigia kura sasa msanii chipukizi Nalimi Mayunga ili arudishe heshima ya ushindi nchini wakati huu anaiwakilisha Tanzania katika fainali za Airtel Trace Music Stars Nairobi machi, 28 2015 katika hotel maarufu ya Enashipai iliyopo jijini humo.

Hayo yamesemwa na Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Bi Aneth Muga katika mkutano maalum na wanahabari kuhusu Fainali hizo za shindano la Airtel Trace Music Stars ambapo lengo lake ni kushirikiana na wasanii wote wanaoziona fulsa na kuzitumia vyema ili kujipatia mafanikio wao pamoja na nchi.
“Airtel tunatamani kuona watanzania  tunaurudisha ushindi nyumbani, Mayunga ni msanii tunaejiamini ataweza kutuwakilisha vyema katika fainali za  Airtel Trace Music Stars kama alivyofanya hapa nchni na akapata nafasi wa kutuwakilisha Tanzania kwenye Fainali za Afrika

“Sasa wote tumpigie kura,1 wasanii wenzake, ndugu, jamaa, na marafiki na wapenda burudani nchini hii ni nafasi yetu ya kushiriki kumpigia kura kijana wetu ili aweze kushinda na kupeperusha Sanaa ya muziki wetu na bendera ya nchi yetu zaidi” alisisitiza Bi. Muga.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando alieleza kuwa kila mwenye laini ya Airtel ataweza kupiga kura awapo mahali popote “

Kumpigia kura Mayunga ni rahisi sana, tuma SMS, yaani ujumbe mfupi andika neno YUN kwenda 15594, au pia unaweza kupiga simu 0901002233 hii itakuwezesha kusikiliza nyimbo zote na kuamua kuchagua nani wakumpigia kura.

“Maandalizi mengine kwa msanii wetu yanaendelea chini ya wataalamu mbalimbali ili kuweka sauti yake fiti, na kujianmini awapo jukwaani, pia mshindi huyu ameshalipwa  zawadi yake ya shilingi milioni 50  na sasa ni  kumpa ushirikiano wa kumpigia kura tu” Alieleza Mmbando.

Nchi nyingine 13 zinazoshiriki mashindano haya barani Afrika ni pamoja na Kenya, Uganda Zambia, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, The Democratic Republic of Congo (DRC), na Gabon.

Mashindano ya Fainali ya Airtel Trace stars yanatarajiwa kufanyika machi 28 jijini Nairobi Kenye katika hotel ya Enashipai huku mgeni wa heshima katika fainali hizo akitarajiwa kuwa msanii Nguli wa kimataifa Akon.

Airtel inaendesha mashindano haya ya kuibua na kukuza vipaji Afrika ambapo wasanii toka nchi mbalimbali wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji vya kuimba kisha kuchujwa na kuchagua msanii mmoja kila nchi anaeiwakilisha nchi yake katika fainali za mashindano na mshindi kupewa dili la kurekoni nyimbo zake akiwa na msanii nguli wa kimataifa
na katika studio za kimataifa huko Marekani.

No comments:

Post a Comment