TANGAZO


Sunday, March 8, 2015

Wanawake wa MSD washerehekea Siku ya Wanawake Duniani kwa aina yake

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (MSD), Bw. Cosmas Mwaifani akifungua sherehe za Siku ya Akina Mama Duniani zilizofanyika.
Bw. Mwaifani akimkaribisha mgeni rasmi wa sherehe hizo, Bi.Helen Mwakipunda ambaye ni Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Bi. Mwakipunda akizungumza na wafanyakazi wa (MSD) wakati wa sherehe hizo.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akina kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili,.Matlida Ngarina aliyeAlikwa kwa ajili ya kutoa mada kuhusiana na magonjwa ya akina mama, akizungumza na wafanyakazi wa (MSD)
 Mjasiriamali maarufu wa saluni jijini Dar es Salaam, Maza Sinare akitoa mada kuhusu ujasiriamali wakati wa sherehe hizo. Sinare alialikwa mahususi kwa ajili ya kuwafundisha akina mama wa MSD namana wanavyoweza kuanzisha biashara zao huku wakiendelea kufanya kazi.
Dr. Chris Mauki, akiwazungumza na akina mama wa MSD namna wanavyoweza kukabiliana na msongo wa mawazo sehemu ya kazi 
 Afisa Habari wa (MSD),Etikusi Siluka ambaye siku hiyo alikuwa msheheshaji wa sherehe hizo akizungumza jambo
Mmoja wa wafanyakzi wa (msd) akimuuliza swali, Dk. Ngarina kuhusiana na uvimbe wa titi kwa wanawake.
Mfanyakazi wa (MSD), Gendi Machumani akimuuliza swali Dk. Ngarina kuhusiana na magonjwa ya njia ya uzazi kwa mwanamke.
Baadhi ya wafanyakazi wa (MSD), wakimsikiliza kwa makini Bi, Mwakipunda aliyekuwa mgeni rasmi.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo, Bi. Mwakipunda akicheza muziki wa Nani Kama Mama wakati wa sherehe hizo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (MSD), Bw. Mwaifani akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa (MCD) pamoja na mgeni rasmi kulia kwake, Bi. Mwakipunda.
Wafanyakazi wa (MSD) ambao wapo kwenye Club ya mazoezi ya MCD, wakifanya mazoezi katika sherehe hizo.
 Wafanyakazi wa hao wakiwapigia makofi wenzao waliokuwa wakifanya mazoezi ya viungo.

Na Blogu za Mikaoni
IKIWA leo ndiyo Siku ya Wanawake Duniani, wanawake wa Ghala la Kuhifadhi Madawa la Taifa (MCD) jana walisherehekea siku hiyo kwa aina yake baada ya kuifanya katika eneo lao la kazi.

Akizungumza na akina mama hao, Victoria Elangwa ambaye ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, alisema wameamua kufanyia sherehe hizo eneo la kazi ili akina mama hao wapewe elimu kuhusu afya ya uzazi, ujasirimali pamoja na kukabiliana na msongo unaowakabili wafanyakazi katika maisha yao ikiwa ni pamoja na sehemu ya kazi.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (mcd),  Bw. Cosmas Mwaifani akifungua sherehe hiyo kabla ya kumkabribisha mgeni rasm, Bi. Helen Mwakipunda ambaye ni Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, aliwapongeza akina mama hao kwa kuadhimisha sherehe hiyo kwa aina ya tofauti.
"Nawapongeza kwa kuamua kuadhimisha siku yenu kwa kuwaalika watoa mada ya afya, ujasiramali na msongo unaoweza kumkabili mtu akiwa kazi na nyumbani," alisema mkurugenzi huyo.
Naye mgeni rasmi, Bi. Mwakipunda aliwapongeza akina mama hao na kuwaambia wazidi kujitokeza katika nafasi mbalimbali za uongozi  kwa sababu wanaweza.


"Hivi sasa wanawake tumeweza kupigania haki zetu mbalimbali na kuondokana na ukandamizwaji uliokuwepo huko nyuma wa kutoshirikishwa kwenye masuala ya mirathi na mambo mengine," alisema Mwakipunda.


Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akina wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Matlida Ngarina akitoa mada ya juu ya magonjwa ya aliwata akina mama kuwa na utamaduni wa kujichunguza matiti yao mara kwa mara ili kubaini kama kuna uvimbe wowote.


Dk. huyo aliongeza kuwa, kufanya hivyo kutawasaidia kujiepusha na kansa ya ziwa ambayo imekuwa aikiua wanawake wengi hivi sasa.


Aliwaeleza wanawake hao maradhi mbalimba ya via vya uzazi na kuwashauri wawape somo mabinti zao wasijihusishe na mapenzi wakiwa na umri mdogo kwani baadaye hupatwa na saratani ya kizazi. 

No comments:

Post a Comment