Hamis Tambwe wa Yanga, akikimbilia mpira na beki wa Simba, Juuko Murshid, wakati wa mchezo huo.
Mchezaji Danny Mrwanda, akiwatoka beki wa Simba, Kessy Ramadhan (4), wakati wa mchezo huo.
Mchezaji Danny Mrwanda wa Yanga, akiwania mpira na beki wa Simba, Kessy Ramadhan (4), wakati wa mchezo huo.
Mchezaji Kessy Ramadhan wa Simba, akimnyanyua Danny Mrwanda wa Yanga, wakati wa mchezo huo.
Mchezaji Kessy Ramadhan wa Simba, akimsidia kumnyanyua Danny Mrwanda wa Yanga baada ya kudondoka wakati walipokuwa wakipambana kuwania mpira.
Mashabiki wa Simba wakionesha furaha yao wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga, wakiwa wamejipaka rangi mwilini, wakiwa na nyuso za huzuni baada ya timu yao kufungwa bao 1-0 na mahasimu wao, Simba, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mashabiki wa Yanga wakiwa na nyuso za huzuni baada ya timu yao kufungwa bao 1-0 na mahasimu wao, Simba, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mwamuzi akimuonesha kadi ya njano beki wa Yanga, Kelvin Yondani wakati wa mchezo huo.
Jonas Mkude wa Simba, akiwa ameshikwa na Said Juma wa Yanga wakati wa mchezo huo.
Said Juma wa Yanga, akijaribu kumzuia Jonas Mkude wa Simba, wakati wa mchezo huo.
Hadi kipindi cha kwanza kinaisha ubao wa matangazo ulikuwa ukionesha mabao yalikuwa ni 0-0.
Wachezaji wa Yanga wakitoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kabla ya kuingia uwanjani kuanza kipindi cha pili.
Wachezaji wa Simba wakitoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kabla ya kuingia uwanjani kuanza kipindi cha pili.
Mashabiki wa Yanga wakiwa wamekaa na sanamu lao kwenye jukwaa lao la upande wa Kusini mwa Uwanja wa Taifa, wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga wakionesha furaha yao kabla ya kufungwa bao na Emmanuel Okwi wa Simba katika kipindi cha pili cha mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la pekee lililofungwa na Emmanuel Okwi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya mahasimu wao wa jadi Yanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Ubao wa matangazo ukionesha Simba bao 1 na Yanga 0, baada ya Emmanuel Okwi kuifungia timu yake ya Simba bao katika mchezo huo.
Mchezaji Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba, akijaribu kumpiga chenga Oscar Joshua wa Yanga wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga wakianza kuondoka kwenye majukwaa ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo baada ya kuona muda ukiyoyoma bila kuwa na matumaini ya kurejesha bao hilo..
Kocha wa Simba, Goran Kopunovic, akifurahia baada ya kumpira kumalizika uwanjani hapo leo jioni.
Kocha wa Simba, Goran Kopunovic, akionesha furaha yake baada ya timu yake hiyo kuipa kichapo cha bao 1-0 timu ya Yanga. Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo jioni.
Mashabiki wa Simba wakifurahia baada ya kumalizika kwa mchezo huo huku timu yao ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga. |
No comments:
Post a Comment