TANGAZO


Wednesday, March 11, 2015

Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba watakiwa kujiunga katika vikundi ili kujikwamua na Umaskini

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dk. Kone akiongea na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana Dk.Steven Kissui na wa kwanza upande wa kushoto kutoka mbele ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi Ester Riwa. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kutoka Idara ya Mandeleo ya Vijana Dk. Steven Kissui aliyenyoosha mikono akielezea jambo kwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Iramba kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Halima Mpita akiongea na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Micheo ambao upo Wilayani humo katika kuvijengea uwezo vikundi vya Vijana ili waweze kujikwamua na umasikini. 
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akiongea jambo na Washiriki kutoka Vikundi mbalimbali vya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ikiwa ni sehemu ya juhudi za Wizara kuwajengea uwezo vijana.

No comments:

Post a Comment