Mh.Naimi Azizi Balozi wa
Tanzania Nchini Ethiopia (Katikati) na Dkt. Hamis Mwinyimvua (kushoto)
wakifurahia jambo na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 8 wa Watalaamu wa
masuala ya Fedha wa Afrika baada ya ufunguzi wa Mkutano huo.
(Na Mpiga Picha wetu)
Na Mwandishi wetu
Tanzania inashiriki mkutano
wa nane wa Wataalamu wa Fedha, Uchumi na
Mipango kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU)
na Kamisheni ya Uchumi ya Afrika (ECA) umeanza nchini Ethiopia kwa
kuwakutanisha wataalamu mbalimbali wa masuala ya Fedha kutoka nchi wanachama wa
Umoja wa Afrika.
Mkutano huo wa watalaamu ni maandalizi
ya Mkutano wa Mawaziri wa Fedha, Uchumi na Mipango wa Afrika ambao utafanyika
kuanzia Machi 30 hadi 31 mwaka huu Addis Ababa nchini Ethiopia.
Katika Ufunguzi wa Mkuatano
huo Mh. Abraham Tekeste,Waziri wa Fedha na Uchumi wa Ethiopia alisisitiza kuwa
umakini unatakiwa katika utekelezaji wa sera tulizojiwekea, vipaumbele na
mikakati ya maendeleo ya kifedha kabla ya kikao cha malengo ya maendeleo
endelevu kitakachofanyika Septemba ,2015.
Mkutano huo ambao pamoja na
mambo mengine utajadili kanuni na utaratibu wa kamati ya watalaam wa masuala ya
fedha, Uchumi na Maendeleo na maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Afrika, utatanguliwa
na uchaguzi wa Mwenyekiti wa kamati ya wataalam na kamati ya Mawaziri wa Fedha,
Uchumi na Mipango wa nchi wanachama wa AU,
na ECA.
No comments:
Post a Comment