TANGAZO


Tuesday, March 3, 2015

Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal aagana na Balozi wa Japana anayemaliza muda wake

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakati akimkaribisha Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 2, 2015. Balozi Okada alifika ofisini kwa Makamu kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. (Picha zote na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 2, 2015, kwa ajili ya mazungumzo na kumuaga rasmi baada kumaliza muda wake wa kazi nchini. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na Balozi wa Japan nchini Tanzania, aliyemaliza muda wake wa kazi, Masaki Okada, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Okada alifika ofisini kwa Makamu kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. 

No comments:

Post a Comment