TANGAZO


Sunday, March 8, 2015

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ziarani Dodoma Mjini

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa amebeba maji kwenye madumu aliposhiriki umwagiliaji maji katika shamba nyanya la vijana wajasiriamali wa CCM katika Kijiji cha Nkulabi, Kata ya Mpunguzi, Jimbo la Dodoma Mjini jana, wakati wa ziara yake, mkoani Dodoma. Kinana yupo mkoani Dodoma kwa ziara ya siku tisa ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiandika jambo muhimu alipokuwa akijadiliana na Viongozi wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu kwenye mkutano na wanafunzi wa vyuo vilivyopo Dodoma jana, wakati wa ziara yake Mkoa wa Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Christopher Ngubiagai na Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa Mkoa wa Dodoma, Steven Lwitiko.
Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Mkoa wa Dodoma, wakiwa wamesimama kwa dakika moja kumuombea dua aliyekuwa Kiongozi wa Kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT), marehemu Kapteni John Komba aliyefariki dunia wiki iliyopita na kuzikwa nyumbani kwao Lituhi, Mkoa wa Ruvuma.Walifanya hivyo walipokuwa kwenye mkutano na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu mjini Dodoma juzi.
Kikundi cha ngoma za utamaduni wa kabila la Wagogo, cha Nuru, kikitumbuiza wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili  katika Kata ya Nzuguni, Jimbo la Dodma Mjini, kushiriki ujenzi wa mradi wa maji jana.
Komredi Kinana akishiriki kuchimba mtaro katika ujenzi wa mradi wa maji katika Kata ya Nzuguni, Jimbo la Dodoma Mjini jana.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa 
Barafu, Mjini Dodoma jana, ambapo alielezea ukigeugeu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwa kuhamasisha wananchi kutojiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kususia kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa wakati huo huo viongozi wao wakiendelea kuhamasisha watu kujiandiksha.

Baadhi ya akina mama waliojiunga na CCM wakila kiapo cha chama hicho wakati wa mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya Barafu, mjini Dodoma jana. (Picha zote na Richard Mwaikenda)

No comments:

Post a Comment