TANGAZO


Tuesday, March 3, 2015

Kampuni ya Rex Energy yazindua teknolojia ya umeme wa jua wa gharama nafuu

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua ya Rex Energy, Francis Kibhisa, akizungumza wakati wa uzinduzi wa nishati ya umeme jua wa gharama nafu wa 3G, Dar es Salaam leo. Katikati ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni mshirika ya Solaric, Didar Islam kutoka Bangladesh. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)  
Mkurugenzi wa Kampuni mshirika ya Solaric, Didar Islam kutoka Bangladesh, akizungumza wakati wa uzinduzi wa nishati hiyo ya 3G.  
Mkurugenzi wa Kampuni mshirika ya Solaric, Didar Islam kutoka Bangladesh, akizungumza wakati wa uzinduzi wa nishati hiyo ya 3G.  
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele (katikati), akizungumza wakati alipokuwa akizindua nishati ya umeme jua wa gharama nafu wa 3G, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua ya Rex Energy, Francis Kibhisa na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni mshirika ya Solaric, Didar Islam kutoka Bangladesh.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele (katikati), akizungumza wakati alipokuwa akizindua nishati ya umeme jua wa gharama nafu wa 3G, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua ya Rex Energy, Francis Kibhisa na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni mshirika ya Solaric, Didar Islam kutoka Bangladesh. 
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele (katikati) akimpongeza Mkurugenzi wa Kampuni mshirika ya Solaric, Didar Islam kutoka Bangladesh, mara baada ya kuzindua nishati ya umeme jua wa gharama nafu wa 3G, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua ya Rex Energy, Francis Kibhisa, iliyozindua nishati hiyo.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele (katikati), akiwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua ya Rex Energy, Francis Kibhisa na Mkurugenzi wa Kampuni mshirika ya Solaric, Didar Islam kutoka Bangladesh, wakionesha vifaa vya 3G vya umeme jua, wakati akizindua nishati ya umeme jua wa bei nafu wa 3G, Dar es Salaam leo.  
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua ya Rex Energy, Mhandisi Arnold Swai, akimuonesha Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele (wapili kushoto), jinsi kifaa cha 3G cha umeme jua, kinavyofanya kazi, mara baada ya kuizindua nishati ya umeme jua wa bei nafuu wa 3G, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni hiyo, Francis Kibhisa na watatu ni Mkurugenzi wa Kampuni mshirika ya Solaric, Didar Islam kutoka Bangladesh. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua ya Rex Energy, Mhandisi Arnold Swai, akimuonesha Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele (wapili kushoto), jinsi kifaa cha 3G cha umeme jua, kinavyofanya kazi kwa kuweza kuwasha kompyuta mpakato pamoja na taa. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua ya Rex Energy, Mhandisi Arnold Swai, akiwasha kompyuta mpkato kwa nguvu ya nishati hiyo ya 3G. 
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua ya Rex Energy, Mhandisi Arnold Swai, akionesha paneli ya Sola inayotumia nishati hiyo ya 3G.
 Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa nishati ya umeme jua wa gharama nafu wa 3G, Dar es Salaam leo, nishati inayosambazwa na Kampuni ya usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua ya Rex Energy ya jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi huo wa nishati ya umeme jua wa gharama nafu wa 3G, Dar es Salaam leo.

Na Mwandishi wetu  
KAMPUNI ya usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua ya Rex Energy, imezindua teknolojia mpya ya gharama nafuu ya umeme kwa matumizi ya nyumbani.

Teknolojia hiyo ijulikanayo kama 3G+Solar Homes System (SHS) ni ya kwanza kutumika Tanzania. Ilizinduliwa Dar es Salaam leo na Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele.

Akizindua nishati hiyo, Kiwele alisema kampuni hiyo imeonesha mfano bora kwa kuzindua mfumo huo wa bei rahisi ili kuwafikia wananchi wa kawaida hususan wa vijijini.

Kiwele alisema uzinduzi huo ni moja ya jitihada za Serikali kuwasaidia wasiofikiwa na gridi ya taifa, hivyo ni utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Francis Kibhisa alisema teknolojia hiyo ni ya kisasa na imebuniwa na mshirika wa Rex Energy, Kampuni ya Solaric PVT Ltd ya Bangladesh.
Pia alisema kuwa umeme huo utapatikana kwa gharama ya sh. 200,000, sh. 300,000 na sh. 400,000, ambapo mteja anaweza akalipa kwa kuanzia na sh. 80,000 na nyingine akalipa kwa mwezi kiasi sh. 20,000 na kuendelea kwa njia za Max Malipo, Tigo Pesa, M-Pesa, Z Pesa na huduma nyingine.

Aidha, Mkurugenzi Kibhisa alisema kuwa watakuwa wakisambaza huduma hiyo sehemu mbalimbali, zikiwemo za mikoani kwa kumia Mawakala wao watakaokuwepo katika sehemu mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment