TANGAZO


Monday, March 9, 2015

Balozi wa Uingereza nchini amtembelea Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli ofisini kwake jijini Dar es Salaam

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akimkaribisha Balozi wa Uingereza nchini Bi Dianna Melrose ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Bi. Dianna Melrose ofisini kwake jijini Dar es Salaam kujadiliana mambo mbalimbali yahusuyo Miundombinu ya Barabara za juu (flyovers), madaraja ya chuma (mabey bridges) na suala zima la kupunguza msongamano katika jiji la Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akisalimiana na Richard Boulter kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimatifa ya Uingereza (Department for International Development) aliyeambatana na Balozi wa Uingereza nchini Bi. Dianna Melrose.
Majadiliano yakiendelea kati ya Ujumbe wa Balozi wa Uingereza nchini, Bi Dianna Melrose pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli. 
Ujumbe kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini, wakwanza kulia ni Balozi wa Uingereza Dianna Melrose, anayefuatia ni Meneja wa Masula ya Biashara na Maendeleo Marie Strain pamoja na Richard Boulter kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimatifa ya Uingereza. (Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU)-Wizara ya Ujenzi)

No comments:

Post a Comment