TANGAZO


Monday, March 9, 2015

Balozi Seif Iddi awataka Watendaji wa Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja kuacha kuyafumbia macho matatizo yanayoibuka katika utendaji wao wa kazi

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na watendaji wa wodi ya wagonjwa wa Kifua Kikuu alipofanya ziara ya ghafla katika Hospoitali Kuu ya Mnazi mmoja kuangalia hali ya usafi wa vyoo kwenye Wodi hiyo. Kulia kwa Balozi Seif ni Mhandisi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Yahya Makame Ameir.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na watendaji wa wodi ya wagonjwa wa Kifua Kikuu alipofanya ziara ya ghafla katika Hospoitali Kuu ya Mnazi mmoja kuangalia hali ya usafi wa vyoo kwenye Wodi hiyo. Kulia kwa Balozi Seif ni Mhandisi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Yahya Makame Ameir. 
Balozi Seif akiangalia hasara ilizozikumba baadhi ya nyumba zilizoathirika kwa upepo katika Jimbo la Kwamtipiura Mjini Zanzibar. Kulia kwa Balozi Seif ni Sheha wa Shehia ya Kwamtipura Bwana Machano Salum Khamis, Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Mh. Hamza Hassan Haji  na kushoto yake ni Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Kheir Khamis. 
Balozi Seif alionyesha masikitiko yake wakati akiiangalia moja ya nyumba zilizopatwa na maafa ya upepo iliyopo pembezoni mwa skuli ya Msingi ya Kwamtipura. 
Balozi Seif akiwafariji baadhi ya wananchi wa Jimbo la Kwamtyip[ura ambao Nyumba zao zimepata maafa ya Upepo mkali uliovuma juzi na jana mchana. 
Balozi Seif akimkabidhi vyakula va baadhi ya Vifaa Sheha wa Shehia ya Kwamtipura Bwana Machano Salum Khamis kwa ajili ya kuwafariji wananachi  waliopatwa na janga na maafa ya upepo Kwamtipura. Kulia kwa Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi. 
Balozi Seif akimkabidhi vyakula va baadhi ya Vifaa Sheha wa Shehia ya Kwamtipura Bwana Machano Salum Khamis kwa ajili ya kuwafariji wananachi  waliopatwa na janga na maafa ya upepo Kwamtipura. Kulia kwa Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi. (Picha zote na Hassan Issa– OMPR – ZNZ) 

Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
9/3/2015.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaagiza  watendaji wa Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja kuacha  tabia ya kuyafumbia  macho matatizo yanayoibuka katika utendaji  wao wa kazi na badala yake waiarifu Serikali Kuu ili hatua za dharura zichukuliwe katika kuyakabili matatizo hayo.

Alisema kuendelea kuyaacha matatizo hayo yasambae mbali ya  kuchafua mazingira lakini pia yanaweza kusababisha maambukizi ya maradhi na kuwaongezea wagonjwa mtafaruku unaoweza kuepukika.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo alipofanya ziara ya ghafla kuangalia hali ya usafi sehemu ya vyoo vya  wodi ya wagonjwa wa Kifua Kikuu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.

Ziara hiyo ya Balozi Seif  imekuja kufuatia Taarifa za Shirika la Utangazi Zanzibar      { ZBC } zilizoelezea hali isiyoridhisha katika sehemu hizo ambayo ilileta mtafaruku kwa Wagonjwa walioazwa kwenye wodi hiyo.

Balozi Seif alisema yeye kama Kiongozi  Mkuu wa shughuli za Serikali atakuwa tayari wakati wowote kutoa msaada  au ushauri wake katika kutanzua matatizo ambayo Viongozi wa  Taasisi hiyo wameshindwa kuchukuwa hatua.

Alisema Wagonjwa pamoja na wananchi wamekuwa  wakilalamikia kero, changamoto na  hata matatizo yanayowakabili katika kupata huduma za afya kwenye  Hospitali ya Mnazi Mmmoja ambayo yamekuwa yakisababishwa na baadhi ya watendaji wazembe.

“ Msifikie pahala mkawa na tabia ya kuvilaumu  vyombo vya Habari kwa kuwapasha Habari Wananchi  juu ya uzembe mnaoendelea kuufanya katika maeneo yenu ya Kazi “. Alionya Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea kwamba Vyombo vya Habari vitaendelea kuwa na haki  na wajibu wa kutoa Taarifa kwa umma matukio ya uzembe unaofanywa na baadhi ya watendaji hao.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifanya ziara ya kuwafariji wananchi wa Jimbo la Kwamtipura ambao nyumba zao zimeathirika kwa upepo mkali uliovuma ghafla juzi na jana mchana.

Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar alipata wasaa wa kuziangalia Nyumba sita za wananchi hao ambazo baadhi yake zimeezuka kabisa mapaa yake.

Sheha  wa Shehia ya Kwamtipura Bwana Machano Salum Khamis { Mbonga } alimueleza Makamu wa ili wa Rais Kwamba upepo huo uliovuma juzi na jana mchana umeezua baadhi ya mapaa nyumba sita ambazo nyengine zimepata athari na kuta zake.
Sheha Machano alisema uongozi wa Shehia ulikutana na waathirika hao kuanza kufanya tathmini ya hasara ya nyumba zilizopatwa na maafa hayo na kuchukuwa hatua za dharura  za uhifadhi wa familia hizo.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipuira Mh. Hamza Hassan Juma alisema Uongozi wa Kamati ya Jimbo la Kwamtipura , wananchi na familia zilizopatwa na maafa hayo zilishirikiana pamoja katika kujaribu kurejesha hali ya kawaida ya mazingira ya nyumba hizo.

Mh. Hamza alisema hatua hiyo iliyochukuliwa ya  dharura kwa pamoja imeweza kuleta  faraja  kwa familia hizo kurejea katika mazingira ya hali ya kawaida.

Akizungumza na familia za waathirika wa maafa hayo ya upepo katika skuli ya Maandalizi ya Kwamtipura Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif aliwataka Wananchi hao mkuwa na subira katika kipindi hichi cha maafa.

Balozi Seif aliyeambatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na kugawa sadaka kidogo kwa familia za maafa hayo alisema ameshtuka mara baada ya kusikia tukio hilo lililoleta hasara kubwa kwa familia hizo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  amewashukuru Wananchi na watu wenye uwezo kwa moyo wao waliouonyesha  katika kujaribu kusaidia familia hizo wakati wa tukio hilo.

Alisema linapotokeza tatizo miongoni kwa mmoja kati ya jamii ni vizuri tatizo hilo likawa na watu wote katika kulitafutia ufumbuzi wa pamoja na si vyema kwa baadhi ya watu kufurahia majanga yanayowapata wenzao kwa sababu tu za itikadi za kisiasa.

No comments:

Post a Comment