Vijana Manispaa ya Kigoma Ujiji wahamasishwa kuchangamkia fursa za Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambaye
pia ni Mkuu wa Idara ya Maendleo ya Jamii Bw. Xavier Keebwe akizungumza wakati
wa ufunguzi wa mafunzo kwa vijana kuhusu Sera ya maendeleo ya Vijana, Stadi za
Maisha,Ujuzi, Mwongozo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana yaliyotolewa na
wawezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambapo jumla
ya zaidi ya Vijana 60 kutoka katika halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji,
Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijini mafunzo hayo yamefanyika
katika ukumbvi wa manispaa hiyo. Kutoka Kulia ni Afisa Vijana kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga na katikati ni Mkuu wa
Kitengo cha Sheria na Mwezeshaji mkuu wa mafunzo hayo kutoka wizara hiyo Bibi.
Esther Riwa.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akitoa mada mbele ya Vijana kutoka
Halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Wilaya ya Uvinza na Kigoma
Vijijini katika warsha iliyofanyika leo
katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Ofisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada mbele ya Vijana kutoka
Halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Wilaya ya Uvinza na Kigoma
Vijijini katika warsha iliyofanyika leo
katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Ofisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada mbele ya Vijana kutoka Halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijijini katika warsha iliyofanyika leo katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Baadhi ya Vijana wakifuatilia mada wakati wa warsha
biliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya
kuhamasisha vijana kuhusu Mfuko wa maendeleo y Vijana nchini. Warsha hiyo imefanyika
leo katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo jumla ya zaidi ya vijana
60 kutoka katika halmashauri za Manispaa hiyo, Wilaya ya Uvinza na Kigoma
Vijijini.
Ofisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Kikundi
cha Peace Group kilichopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Bibi. Cecilia
Alphonce walipotembelea kikundi hicho kwa ajili ya kukagua shughuli zao leo
mkoani Kigoma.Kikundi hicho kinajishughulisha na uzalishaji wa miche ya miti na
maua na kinaundwa na wanachama watano.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Bibi. Esther Riwa akisikiliza maelezo kuhusu uzalishaji wa miche ya
maua kutoka kwa mmoja wa wanakikundi cha Peace Group kutoka Manispaa ya Kigoma
Ujiji Bibi. Angelina G. Masunzu leo wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Vijana
mkoani Kigoma.
Ofisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akijaribu namna mashine ya kuchana mbao
inavyofanya kazi walipotembelea Kikundi cha Vijana cha Ubhumwe Carpenter
Cooperative cha mjini Kigoma leo. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa kikundi hicho
Bw. Gasto Yagaza.
Karani wa Kigoma Youth Entrepreneur Saccos
Bibi.Fatuma Hamisi akisoma taarifa ya Saccos hiyo mbele ya Wataalamu kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipotembela katika ofisi za
Saccos hiyo leo mjini Kigoma. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Saccos hiyo Bw.
Kapele Shaban, Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Amina Sanga, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara
hiyo Bibi. Esther Riwa na Katibu wa Saccos hiyo Bw. Ramadhan Daud.
Wataalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa (katikati) na Afisa Vijana wa Wizara
hiyo Bibi. Amina Sanga (kushoto) wakiangalia nyaraka za usajili wa Saccos ya
Kigoma Youth Entrepreneur Saccos iliyopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji leo.
Kulia ni Katibu wa Saccos hiyo Bw. Ramadhan Daud. (Picha zote na Frank Shija,
WHVUM)
No comments:
Post a Comment