Mwanahabari Frank Kibiki, aliyewahi kuwa Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ngazi ya Wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa NEC.
Fredrick Mwakalebela akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Na mwanahabari wetu Fredy Mgunda,Iringa.
WANANCHI na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Manispaa ya Iringa wameendelea na sitofaham la nani ni mtu sahihi wa kugombea jimbo la Iringa Mjini kutokana na wagombea wengi kujitokeza katika harakati hizo.
wakizun gumza kwa nyakati tofauti wananchi na wanachama hao wamesema kuwa kuna watu ambao tayari wamejijengea majina katika harakati hizo ambao na Jesca Msambatavangu, fredrick mwakalebela na mahamood madenge wote wanasadikika kuingia kwenye kinyang’anyilo hicho.
Ila mwanahabari Frank Kibiki, aliyewahi kuwa Katibu wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ngazi ya Wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni Mjumbe wa NEC ameonekana kuvurunga kabisa plani za wanachama kutokana na kuoneka ni kiongozi anayefaa kuigwa na kila rika inayomzunguka.
Wakizunguza kwa nyakati tofauti wanachama wa CCM, wamesema kuwa Frank Kibiki ndiye mtu pekee anayeweza kuleta upinzani kwa Mbunge wa Jimbo hilo, Mchungaji Peter Msigwa kutokana na kujiamini kwake.
Wameongeza kwa kusema kuwa Frank Kibiki anaushawishi mkubwa kwa jamii tofauti na watu wengine wanaopanga kugombea jimbo hilo, kwasababu anasiasa safi na sera ambazo zinatekelezeka kulingana na mazingara ya wananchi wa Manispaa ya Iringa.
Pia waliongeza kuwa wananchi wanahamu ya kumfahamu Frank Kibiki kutokana na jina lake kukua kwa ghafla na kuwaguza wanachi wengi hivyo inapelekea siku hadi siku kumtafuta na kutaka kumjua yeye ni nani na anafanya nini.
Walimalizia kwa kusema kuwa Kibiki ni mtu pekee ambaye anaweza kuwaweka Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja kutokana na kutokuwa na kundi hata moja ndani ya chama tofauti na wagombea wanaotarajiwa kugombea jimbo hili.
Kwa upande wake Katibu wa CCM, mkoani Iringa Hassani Mtenga alisema kuwa ipo siku kwenye kura za maoni watu watazimia, hii ni kutokana na baadhi ya watu wanaotarajia kugombea jimbo hili wamekuwa wakitumia pesa nyingi kuwahonga wananchi ili wamchague na akasisitiza kuwa uongozi sio pesa uongozi ni kipaji na uwezo wa mtu binafsi aliopewa na Mungu.
No comments:
Post a Comment