Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt Lu Youqing akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa Bernard Membe kutoa hotuba kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe ya mwaka mpya wa Kichina jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimatafa Bernard Membe akizugumza jambo na Balozi wa China
nchini Tanzania, Dkt Lu Youqing wakati
wa sherehe ya mwaka mpya wa Kichina iliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa Bernard Membe(kushoto) na Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. LU Youqing (katikati) wakati wa sherehe ya mwaka mpya wa Kichina iliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Meck Sadiki.
Balozi wa China nchini
Tanzania, Dkt Lu Youqing (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick
Meck Sadiki (kulia) wakicheza ngoma ya iliyoimbwa kwa
lugha ya Kishwahili na Kichina inayosema tupige jahazi iende mbali wakati
wa sherehe ya mwaka mpya wa Kichina iliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waliaohudhuria sherehe ya mwaka mpya wa Kichina iliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. (Picha zote na Eleuteri mangi- MAELEZO)
Na Magreth Kinabo na Eleuteri Mangi- MAELEZO
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa, Bernard Membe, ameipongeza Serikali Jamhuri ya China kwa msaada wake wa kuhakikisha Tanzania imefungua idara ya maalum ya upasuaji wa moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam.
Hayo, aliyasema jana viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe ya mwaka mpya wa Kichina.
“Tuna mengi ya kusema kuhusu misaada ya maendeleo inayoletwa na ndugu zetu Wachina Sasa hivi muhimbili, kwa mfamo wametusaidia kufungua idara maalum ya upasuaji wa moyo, ambayo sasa unaweza kufanya upasuaji wa moyo jambo ambalo lilikuwa hadithi ya kufikirika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Lakini sasa hivi Watanzania wanaweza kwenda kutibiwa ugonjwa wa moyo kwa kupasua na kufanyiwa matibabu. Tunawapongeza Serikali ya China kwa kuleta msaada mkubwa wa aina hii nchini Tanzania,” alisema Waziri Membe.
Katika sherehe hizo za mwaka mpya,Jumuiya ya Wachina waishio nchini Tanzania waliungana pamoja na wageni wengine kusherehekea siku kuu hiyo, ambayo itaanza rasmi February 18, mwaka huu.
Waziri Membe akifafanua kuhusu mwaka huo, alisema kuwa utajulikana kama mwaka wa kondoo, ambapo mwaka jana 2014 ulijulikana kama mwaka wa farasi.
Jumuiya hiyo wamechagua siku hiyo ya Februari 14 kwa kuwa ni mwisho wa wiki tofauti na siku yao rasmi ya mwaka mpya ambayo itaangukuia Jumatano ambayo ni katikati ya wiki na kuwanyima wengine fursa ya kuhudhuria na wanasherehekea siku yao ya mwaka mpya 2015.
Aliongeza misaada mingine ya maendeleo ilitolewa na nchi hiyo ni miradi ya maji Dodoma na Chalinze mkoani Pwani, mradi ya kilimo Dakawa mkoani Morogoro, Uwanja wa Taifa wa Michezo na Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, uliopo jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt Lu Youqing alisema sherehe hiyo kama alama ya kufahamu utamaduni wa nchi hiyo, imeshafanyika kwa mafanikio mkubwa kwa miaka sita nchini Tanzania na inapendeza, ambayo ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta ya utamaduni.
“Uhusiano wa Tanzania na China sasa uko katika kipindi kizuri cha Juu, mwaka 2014 uliopita ni miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na China. Kwa nusu karne uhusiano nchi hizi mbili zinasaidiana na urafiki wa baina ya nchi hizi mbili umepata maendeleo makubwa,” alisema Balozi Dkt Youqing.
Balozi huyo aliishukuru Serikali Tanzania kwa kuunga mkono sherehe hiyo na aliwaomba wananchi wa nchi hizo kushirikiana na kusaidiana ili kupata maendeleo pande zote mbili.
Serikali hiyo ya China imepongezwa kwa kuwa nchi mfano wa kuigwa kwa kutoa misaada mbalimbali Barani Afrika,ambapo imesaidia kutatua migogoro na kutoa dola za Marekani milioni 35 kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola na kutoa madaktari 200 ili kukabiliana na janga hilo katika nchi za Liberia,Guinea pamoja na Sierra Leone .
No comments:
Post a Comment