Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa kuwaenzi Waasisi wa Taifa walipofika kuzungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein leo asubuhi katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar. Kutoka kulia ni Aisha Ali Karume, Asha Kombo Haji na Rase-Mary J. Nyerere. (Picha zote na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiongoza Ujumbe wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa kuwaenzi Waasisi wa Taifa leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani (aliyesimama), akisoma taarifa ya wajumbe wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa kuwaenzi waasisi wa Taifa, wakati wajumbe, walipofika Ikulu, Mjini Zanzibar leo asubuhi. Wengine, wapili kushoto ni Mwenyekiti Vikabenga Nsa Kaisi na Aisha Ali Karume Mjumbe.
No comments:
Post a Comment