TANGAZO


Sunday, February 22, 2015

Raia wa Rwanda na Kenya huru kuingia UG

Bunge la Afrika mashariki
Serikali ya Uganda imeondoa ada ya kibali cha kufanyia kazi nchini humo pamoja na mahitaji ya viza miongoni mwa raia wa Kenya na Rwanda wanaoingia na kutoka taifa hilo.
Uamuzi huo uko sambamba na uidhinishaji wa mtindo wa uhuru wa kutembea chini ya Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Soko la pamoja ambayo iliafikiwa mwaka 2009 na marais Museveni wa Uganda,Mwai Kibaki wa Kenya na Jakaya Kikwete wa Tanzania,Paul Kagame wa Rwanda na Pierre Nkurunziza wa Burundi.
Kamishna wa udhibiti wa uhamiaji katika wizara ya maswala ya ndani bwana Anthony Namara ameliambia gazeti la Monitor jumamosi kwamba raia wa mataifa hayo mawili pia hawatahitajika kutoa viza ama vibali vyovyote vya usafiri ili kuingia Uganda isipokuwa vitambulisho vyao pekee.
Amesema kuwa Kenya na Rwanda tayari zinaidhinisha mpango huo wa uhuru wa kutembea ambao unalenga kuimarisha utalii katika eneo hili mbali na kuruhusu usafiri wa wataalam katika mataifa haya matatu.
Tanzania na Burundi hayamo katika mpango huu unaoshirikisha vibali vya kufanya kazi na mahitaji ya Viza.

No comments:

Post a Comment