TANGAZO


Sunday, February 22, 2015

Kenya na TZ kutatua mgogoro wa kitalii

Utalii
Maafisa wa serikali kutoka Tanzania na Kenya watakutana mjini Arusha mwezi ujao ili kutafuta suluhu ya kutatua mzozo kuhusu marufuku ya magari ya kitalii kutoka Tanzania kuingia katika uwanja wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tangu Disemba mwaka uliopita.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, Katibu wa kudumu katika wizara ya madini, mali asili na utalii Daktari Adelhelm Meru amesema kuwa swala hilo ni la kibiashara na halikuweza kuwasilishwa mbele ya kikao cha marais wa Afrika mashariki kilichokamilika jijini Nairobi.
Rais Uhuru Kenyatta wa kenya
Amesema kuwa mkutano huo utafanyika mjini Arusha mwezi Machi tarehe 18 hadi 20 na anatarajia kupata suluhu ya muda mrefu ya mgogoro huo,ambao huenda ukaathiri uhusiano kati ya mataifa haya mawii ambayo yanashindania Utalii katika eneo hili.
Tangu mwezi Disemba mwaka uliopita,mamlaka ya Kenya iliweka marufuku ya magari yote ya kitalii kutoka Tanzania kutoingia katika uwanja wa Ndege wa Jomo kenyatta Jijini Nairobi ikidai kwamba inaidhinisha makubaliano ya mwaka 1985 na Tanzania kuhusu ushirikiano wa Utalii.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Wakati mmoja waziri wa mali Asili na Utalii Lazaro Nyalandu alilazimika kusafiri jijini Nairobi ili kushauriana na mwenzake wa Kenya ,lakini Kenya ikaondoa marufuku hiyo kwa wiki tatu huku ikitaka kufanyika kwa majadiliano na jirani wake wa kusini.
Inakadiriwa kwamba takriban watu laki 300,000 husafiri kutoka na kuingia Tanzania kupitia Uwanja wa Ndege wa JKIA kila mwaka wakati wanaposafiri maeneo mingine ulimwenguni.

No comments:

Post a Comment