TANGAZO


Saturday, February 28, 2015

Jaji Kiongozi atoa somo kwa Watendaji wa Mahakama ya Kazi, Chama cha Waajiri na Wafanyakazi

Baadhi ya washiriki wa mkutano maalum wa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) wakifuatilia masuala mbalimbali leo jijini Dar es Salaam. 
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mkutano maalum wa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) leo jijini Dar es salaam. 
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila akifungua mkutano maalum wa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) leo jijini Dar es salaam.Mkutano huo unalenga kuangalia na kutafuta majibu ya changamoto mbalimbali zinazohusu maslahi ya wafanyakazi na mashauri yanayopelekwa mahakama Kuu Divisheni ya Kazi nchini. 
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila akifungua mkutano maalum wa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) leo jijini Dar es salaam. Mkutano huo unalenga kuangalia na kutafuta majibu ya changamoto mbalimbali zinazohusu maslahi ya wafanyakazi na mashauri yanayopelekwa mahakama Kuu Divisheni ya Kazi nchini. 
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza jambo na Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila kabla ya kuanza kwa mkutano maalum wa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) leo jijini Dar es Salaam.

Na Aron Msigwa – MAELEZO
28/2/2015. Dar es salaam.
JAJI Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila ametoa wito kwa watumishi na watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi nchini kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, viwango na uadilifu ili mahakama hiyo iendelee kuwa kimbilio la wananchi wanaotafuta haki.

Akizungmza wakati wa wakati wa kikao cha wadau wa Mahakama kujadili uboreshaji wa utendaji kazi katika Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kilichowahusisha watendaji wa Mahakama ya Kazi , Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) leo jijini Dar es slaam, Mhe.Shaaban Lila amesema kuwa  msingi mkuu wa Mahakama ya Tanzania nikuhakikisha kuwa inatoa maamuzi kwa wananchi kwa haki na wakati.
Amesema  iwapo waajiri na wafanyakazi kote nchini watazingatia haki na wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao kulingana na kanuni na taratibu zinazosimamia maeneo yao ya kazi migogoro  mingi inayopelekwa mahakamani baina ya waajiri na wafanyakazi itapungua kote nchini.

“Kila upande ufanye kazi yake kwa kuzingatia  haki ,kumekuwa na mrundikano wa mashauri ya kazi yanayokwenda mahakamani kwa ajiri ya utatuzi na usuluhishi ,mengi ya mashauri hayo hayahusiani kabisa na mfanyakazi kufukuzwa kazi isipokuwa yale yanayohusu  mfanyakazi  kukosa uaminifu, wizi na ubadhirifu sehemu mahali pa kazi” Amesisitiza.

Amesisitiza  kuwa utendaji kazi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi pamoja na maamuzi inayoyachukua katika kutatua na kushughulikia kero na migogoro mbalimbali ya kazi   katika maeneo mbalimbali nchini lazima uheshimime ili kuendelea kujenga taifa linaloongozwa katika misingi ya haki. 

Mhe. Shaaban amesema  watendaji na watumishi wa mahakama lazima waendane na kasi  ya mabadiliko yanayofanyika katika kushughulikia mashauri ya muda mrefu mahakamani na kuongeza kuwa mkakati wa mahakama hiyo ni kuendelea kupunguza umri wa mashauri yaliyoko mahakamani yenye umri kuanzia miaka 3 hadi 10 ili yaweze kushughulikiwa katika kipindi kisichozidi mwaka 1 hadi 2.
“Lengo letu ni kushughulikia mashauri haya haraka na kwa muda mfupi, muhakikishe mashauri haya mnayamaliza kwa sababu yanagusa uzalishaji na maisha ya watu, kuchelewa  kuyasikiliza  kunaathiri  uchumi ” Amesisitiza.

Aidha,amewataka wadau wanaoshiriki mkutano huo kujipima katika malengo wanayojiwekea pamoja na kusimamia utekelezaji wa hukumu na maamuzi yanayotolewa na mahakama na kueleza kuwa ofisi yake inaandaa mkakati wa usimamizi wa suala hilo.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri nchini Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mulimuka akizungumza katika mahojiano maalum amesema kuwa mbali na mkutano huo kuwaweka pamoja wadau  hao kwa maana ya Mahakama, Waajiri (Serikali) na waajiriwa unalenga kuangalia na kutafuta majibu ya changamoto mbalimbali zinazohusu maslahi ya wafanyakazi na mashauri yanayopelekwa mahakama Kuu Divisheni ya Kazi nchini. 
Amesema asilimia 70 ya mashauri yanayokwenda  mahakama Kuu Divisheni ya Kazi yanahusu migogoro ya waajiri  kuwasimamisha kazi wafanyakazi wao kutokana na makosa mbalimbali na kuongeza  kuwa mengi ya makosa hayo hayasababishi mtu afukuzwe kazi.
Ametoa wito kwa pande zote kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ili mashauri yote yanayopelekwa mahakamani yaweze kupatiwa ufumbuzi wa kudumu ili kuondoa migogoro ya kazi inayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment